Soma Marko 10:46-52 na Yohana 5:1-9. Katika matukio hayo yote, Yesu aliuliza maswali. Kwanini alifanya hivyo?
Zingatia katika matukio hayo yote kwamba Yesu aliuliza
walichokuwa wanakihitaji ingawa hitaji lao lilikuwa dhahiri na hata kama
sivyo Yesu angelitambua ni nini yaliyokuwa mahitaji yao.
Hata hivyo kwa kuuliza maswali hayo, Yesu alionyesha
heshima kwa watu, Alionyesha kwamba alikuwa anawasikiliza, kwamba
alijali kuhusu hilo walilokuwa wanakabiliana nalo. Ni masuala mangapi
ambayo watu , labda Zaidi ya kitu chochote huhitaji mtu tu wakuzungumza
naye, mtu ambaye atawasikiliza? Wakati mwingine kuwa na wazo la
kuzungumza juu ya tatizo la mtu inaweza kumsaidia kujisikia vizuri.
Fikiria kwa muda mfupi jinsi gani ungejisikia kama
ungeingia ofisi ya daktari na daktari akakuangalia mara moj tu na
kukuandika dawa na kukutoa nje.Kwa hakika ungekuwa na wasiwasi iwapo mtu
huyo alielewa tatizo lako. “Ungeweza sema daktari hakuniuliza mimi,
jinsi ninavyo jisikia au hata kusikiliza mapigo ya moyo, wala kupima
shinikizo langu la damu au…Mojawapo ya kanuni za utabibu ni kutambua
ugonjwa kabla ya kuutibu.”
Dhana hiyo hiyo inatumika katika shughuli za utume wa
kitabibu,ambayo hulenga katika ustawi wa watu na afya zao na kuwahudumia
katika mahitaji yao kiujumla. Makanisa mengi mno wanafikiri kwamba
wanajua ni nini cha kufanya ilikuwahudumia wengine katika jamii
yao.Wakati sisi tukijitahidi kuzungumza na watu kuhusu mahitaji yao au
mahitaji ya jamii, Huwaonesha kwamba tunajali na hutujulisha sisi kwamba
jinsi gani tunaweza kuwatumikia kwanjia ambazo zitakubalika,pia
tutatengeneza marafiki wapya.
“Kumbuka kwamba unaweza kuvunja upinzani wowote kwasababu
ya maslahi binafsi ya watu unaokutana nao. Kristo alichukulia shauku za
wanaume na wanawake alipokua akiishi nao hapa duniani.Popote alipokwenda
alikuwa mmsionari na mtabibu.Tunapaswa kwenda huku tukitenda mema, kama
alivyotenda. Tumeelekezwa kuwalisha wenye njaa, kuwa visha walio uchi
na kuwafariji wenye huzuni”- Ellen G.White, Welfare Ministry.uk 162.
Wengi wetu hatuna tatizo kuelezea maoni yetu.tunawezaje kujifunza kuwa wasikilizaji bora? ****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment