Soma: Kum. 15:11; Ayu. 29:11-17; Mit.14:31;
Mit.19:17;Mdo.3:6;Yak.1-27; Ellen G.White,
“Pioneering in Australia,
“uk.327-338, kwenye kitabu kiitwacho, Welfare Ministry.
Kama ilivyokuwa kwa Yesu Petro alihusika katika kuwafikia
wahitaji. Tunaweza kuona mfano huu katika kisa cha Paulo katika vilima
vya mars huko Athene. Katika Matendo 17:23, Paulo akiwa amekasirishwa na
ibada za sanamu katika mji ule ,Alijiingiza katika mijadala na wasomi
na watu wowote katika sehemu ya soko,ambaye angezungumza naye.
Aliyatambua mahitaji yao na masuala yao waliyokuwa nayo. Aligundua
kwamba wana nafasi kwa Mungu wasiyemfahamu katika maisha yao na kwamba
wanahitaji kumfahamu Mungu wa kweli na kuacha kuabudu sanamu zisizo na
maana. Kisha akaanza kuhubiri katika masinagogi ambapo wayahudi na
“waliokuwa wanamcha Mungu” (Mdo 17:17) Kwa maneno mengine,yeye aliitumia
fursa hii ilikuwafikia kiinjili hao waliopo nje, Paulo alitaka
kuwafikia huko walipokuwepo, kama tunavyoona jinsi alivyoongea na watu
katika sinagogi na watu walioko katika masoko. Umati wa watu uliamini
uungu wa aina Fulani kwakuwa walikuwa wamejenga mdhabahu iliyokuwa
imeandikwa “kwa Mungu asiyejulikana” (Mdo 17:23).
Na kwa kufanya kazi
Paulo alitafuta kuwaelekeza kwa Mungu, “nawahubiri habaru zake yeye
ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua” (Mdo 17:23) Hata hivyo baadae
alinukuu mmoja wa washairi,aliyetokea kuandika kitu cha ukweli, “ maana
sisi tuwazao wake”( Mdo 17:28). Kwakuanzia mahali watu walipokuwepo
alitaka kuwaongoza kutoka katika sanamu zao na kumwelekea Mungu
anayeishi na Yesu aliyefufuka kutoka katika wafu. Kwa kifupi, tathimini
mahitaji ya wale aliotaka kuwafikia Paulo na kuanzia hapo alijaribu
kuwasaidia kutimiza mahitaji yao.
Maswali ya Mjadala
1. “ Yeye ambaye aliwafundisha watu njia ya kupata Amani na
furaha , alikuwa pia anawapatia uzito wa mahitaji yao ya kiroho.”-
Ellen G.White, The Desire of Ages,uk.365. Ni ujumbe gani wa muhimu
tunaopatiwa hapa kwa kuzingatia kwamba tunapaswa kutoa huduma kwa
mahitaji ya wengine?
2. Kwanini sisi,tunapokuwa tunafikiri kuwafikia
wengine,tunapswa kuwa waangalifu bila kusahau hatma ya lengo letu? Ni
nini hatma ya lengo letu? Toa sababu ya jibu lako.
3. Ni kwa namna gani tutajifunza kuona kuwa baadhi ya
vikwazo siyo usumbufu ila ni fursa kwaajili ya huduma?Ni kwa vipi
Wagalatia 2:20 hutusaidia katika eneo hili?****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment