Wednesday, August 24, 2016

Soma Matendo 9:36-42. Ni nini alichokifanya Dorkasi kule Yafa baada ya kugundua kwamba amezingirwa na wahitaji? Katika Matendo 9:41, Ni nini maana ya kifungu hiki cha maneno, “wanaoamini hasa wajane”?
Dorkasi alikuwa mwanafunzi wa vitendo, “ Katika Yafa kulikua na mwanafunzi mmoja aliyeitwa Tabitha.” (Matendo 9:36). Inaweza kusemwa, ”kwamba katika ( jina la mji wako) kuna wanafunzi ( taja majina yao) ambao wamejawa na “matendo mema na tabia njema” Mdo. 9:36.

“Waaminio” ni washiriki wa kanisa la Kikristo; “wajane” ni pamoja na washiriki wa kanisa na wale ambao sio washiriki. Dorkasi aliwahudumia wote. Yafa yako inapaswa kuwa nje na ndani ya kanisa lako, kujali kwa uthabiti wale walio ndani ya kanisa pia ni uinjilisti wenye nguvu(soma Mdo. 2:42-47). Watu nje wanaweza kusema tazama jinsi hao Waadventsta Wasabato walivyo na upendo na kujali.
Soma Yohana 13:34-35 na Yohana 15:12. Ni nini ujumbe unaopatikana katika maandiko hayo matatu, ni kwanini ni muhimu kwetu kama kanisa kufuata? Ni kwanini wakati mwingine inakuwa ngumu kufuata kwa bidii?
Wakati mipango ya kuwatumikia wa nje ya kanisa lako,unapaswa kufikiria mtindo,mbinu ambayo utatumia.
Amy Sherman anaelezea mitindo mitatu, ambayo kanisa linaweza kutumia katika kuhudumia jamii. Mtindo wa kwanza : mtindo wa Mkazi unalenga katika kukidhi mahitaji ya jamii iliyo karibu kabisa na kanisa lako. Mwanamke aliyekuwa akitoa huduma kwa waathirika wa UKIMWI Alichagua jamii iliyomzunguka “ Yaffa”

Mtindo wa pili, Mtunza Bustani, Mtindo huu humaanisha kuendeleza huduma inayofungamana na maeneo jirani nje ya kanisa lako Kama mtunza bustani anavyoona bustani ni ongezeko tu la nyumba yao, wakati mwingine makanisa kadhaa huungana kuendesha kituo cha huduma kwa jamii nje ya kila jamii inayowazunguka. Katika Mji mmoja makanisa kadhaa wanaendesha huduma ya kuhifadhi vyakula bora, kutokana na mradi huu wameanzisha kanisa lingine jipya.

Mtindo wa Tatu ni Mchungaji wa kondoo; Ni Kuwahudumia idadi Fulani ya kundi moja lililolengwa badala ya makundi madogo madogo ya maeneo tofauti ya kijiografia. Imenukuliwa kutoka Ronald J.Sider na wenzake, Churches that Make a Difference: Reaching Your Community with Good News and Good Works( Grand Rapids, Mich.:Baker Books 2002),uk.146


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA