“Mkabidhi BWANA kazi zako na mawazo yako yatathibitika” Mithali 16:3
Mara kanisa lako linapokuwa na maono thabiti ya jinsi
linavyoweza kuhudumia jamii ni muhimu kuendeleza mpango huo ambapo idara
zote za kanisa zinweza kufanya kazi ili kufanya maono yao yawe ya
kweli, Ingawa unaweza ukajiona wewe sio kiongozi katika kanisa lako,
lakini unaweza ukachangia. Pia ni vizuri kwa washiriki wote wa kanisa
kuelewa mchakato huu, kwakuwa hili linahusu utume wa kanisa lako kwa
jamii.
Kimsingi, mpango mkakati wa kanisa unapaswa kuzingatia
angalau vyanzo vitatu 1: Nyenzo kutoka katika kanuni ya Biblia na Roho
ya unabii 2: Maarifa ya kutambua mahitaji ya kijamii 3: Nyenzo kutoka
katika kwa washiriki. Baadhi ya makanisa yamekusanya nyenzo mbalimbali
kutoka kwa washiriki kwa kupitia tafakuri zao, wakati wanapoalikwa kutoa
mawazo yao,njozi zao kwaajili ya kuwafikia watu wanje na kuboresha hali
zao ndani ya kanisa.
Soma Luka 14:25-35. Je kifungu hiki cha maneno kinahusikaje
kikamilifu na mipango inayohitajiwa ili kutimiza utume wa kanisa lako?
Kama unafikiria kuhusu mchakato unaohitajika ili kukudhi
mahitaji ya jamii yako kwa ufanisi, Unaweza kufikiri: Hili linachukua
uthabiti pamoja na muda. Tungependelea kupitia njia mkato. Mifano miwili
inatonya dhidi ya kuchukua majukumu ya utume na uanafunzi kwa wepesi.
Hutukumbusha kwamba uchambuzi na mipango wa utume wetu ni vya muhimu. Ni
suala la uwakili mwema, ladha ya chumvi katika Luka 14:34, Huwakilisha
ibada. Bila hili, huduma yetu, uanafunzi wetu ni bure na hauna maana.
Tunahitaji kuwa na bidii katika ibada kamilifu na Imani kwa Bwana wetu,
na kama tunayo hiyo bidii na ibada kamilifu huduma pia itafuata.
Je, Ni njia gani ambazo unaweza kufanya Zaidi pamoja na
kanisa lako katika kuandaa na kupanga mapema kabla ya kuifikia jamii
huko nje?****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment