Dr. Taphinez Machibya |
Na Dr. Taphinez Machibya
MFUMO
WA KINGA MWILINI: Ni ukweli ulio dhahiri kwamba kwa msaada wa Mungu, mwili unaweza kujiponya
wenyewe.
Kama vile mwili ulivyo na uwezo wa kukitumia chakula tulacho ili kuweza
kuupatia mwili nguvu,joto, ukuaji na urekebishwaji vivyo hivyo Mwili unazo njia
ndani yake za kuleta uponyaji mara tu mtu apatapo ugonjwa . Natural Remedies
Encyclopedia:Basic Principles of Healing.pg.18
Ni kwa nguvu ya Mungu pekee inayoweza kutufanya na kutuweka salama.
Hakika, ni Mungu ambaye siyo tu alituumba, bali ndiye yeye pia ambaye aliumba
vyakula tunavyo hitaji! Natural Remedies
Encyclopedia:Basic Principles of Healing.pg.18
Mfumo wa
mwili daima hukabiliwa na kuharibika na kuchakaa. Lakini
kuna njia ndani ya mwili ambazo hufanya kazi katika kusafisha,
kurekebesha na kutengenza. Badala ya kutumia nishati na virutubisho
kutoka chakula tulacho katika kumeng’enya chakula na katika misuli n.k, mwili huelekeza
matumizi yake kwa ajili ya kusafisha, kurekebesha, na kujenga upya. - Natural Remedies Encyclopedia:Basic
Principles of Healing.pg.18
Kazi hii
ya usafishaji, urekebeshwaji na kujenga upya,hufanywa kupitia mfumo
wa kinga mwilini.
Mara mtu
anapokuwa mgonjwa, chembechembe hai, viungo, tishu na mifumo ya mwili huwa
chakavu na zilizojawa uchafu na sumu.
Neno
ugonjwa hutafisiriwa toka neno la kiingereza “Dis-Ease” Ambayo
humaanisha mwili “kutokuwa-SawaSawa” - Natural Remedies
Encyclopedia:Basic Principles of
Healing.pg.18
Hivyo ugonjwa
na dalili zake huwa ni matokeo ya asili (nature) katika kuusafisha,
kuurekebesha na kuujenga upwa mwili(Healing Crisis).
Dalili za
ugonjwa kama homa,kukohoa, kuchoka mwili, vipele na majipu, kutokwa jasho,
kupoteza hamu ya kula, usingizi sana, kutapika na kuharisha n.k, vyote hivi
huwa ni sehemu ya uponyaji (Healing Crisis).
Matabibu
na watu wakawaida wamekuwa wakiifahamu hali hii kwa miaka maelfu. - Natural
Remedies Encyclopedia:Basic Principles of Healing.pg.18
KINGA
YA MWILI :
Ni mkusanyiko wa wa chemchembe hai, tishu na ogani za mwili ambazo
huungana pamoja katika kuukinga, kuukarabati na kuujenga upwa mwili dhidi ya
ajari, uchafu, sumu au maambukizi ya wadudu mwilini.
Mwili hupambana na yote hayo:
Kwa kuwa
na uwezo wa kuzitambua hatari/adui
(Antingens)zozote mwilini kama vile: uchafu,sumu,wadudu (bakteria,
virusi,fangasi, minyoo na parasaittari na kuzitoi wowote),na Chembechembe hai
ama tishu zilizo haribika Mf:Chembechembe hai za kansa.
Kwa kuwa
na uwezo wa kuzitofautisha chembechembe hai , tishu na viungo vya mwili vilivyo
salama. (National Institute of Allergy and Infectious
Diseases: Immune System MSD Manual, Consumer Version:Overview of Immmune
System)
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment