Sunday, September 25, 2016

Moja katika matendo ya ukristo ni kufanya huduma kwa jamii, jana katika viwanja vya Hospitali Teule ya Halmashauri ya Shirati waimbaji wainjilisti toka katika kanisa la Waadventista wa Sabato Tegeta jijini Dar Es Salaam walifika katika Hospitali hiyo na walitoa Delivery bed, vifaa tiba,dawa na waligawa khanga kwa kila mgonjwa ndani ya wodi ya kina mama, wodi ya watoto na pia wahudumu walikuwa zamu. Alipokuwa anapokea vifaa hivi toka kwa waimbaji hawa, Mganga mfawidhi wa Hospitali hii Dr. Chirangi aliwapongeza na kuwashukuru sana waimbaji wa Born to Praise. "Kimsigi tuna mahitaji mengi katika hospitali yetu, hata kwenye wodi ya kina mama hata hizi khanga zitakuwa msaada sana hasa kwa wale walikwisha jifungua" alisema Dr Chiragi.
Hii ni moja kati ya mipango ya waimbaji wa Born to Praise katika safari yao iliyoanzia Dar Es Salaam kwenda Shirati na leo wapo kwenye tamasha la uwekwaji wakfu wa DVD namba 2 ya kikundi cha Lake Zone Voice ha ikumbukwe waimbaji hawa kama blog yetu ilivyotaarifu hapo awali kuwa katika safari hii wanafanya kazi ya utengenezaji wa DVD yao namba moja ya PEPETO chini ya Infinite Production na Injilileo Blog chini ya Shua Media & General Enterprises watakuletea yote usiyoyajua juu ya kikundi hiki. 


Mwenyekiti wa Kikundi cha Born to Praise Naftal Phillip Nyambita alijitambulisha kwa Dr Chirangi na kuwatambulisha waimbaji wa Born to Praise nae alisema kidogo juu ya vifaa walivyoleta waimbaji hawa ikiwemo vifaa tiba, madawa, khanga ambazo ziligawawiwa kwa wodi ya kina mama, wodi ya watoto na pia wahudumu wa zamu siku ya jana.


Katibu wa kikundi cha Born to Praise Bambino Phillip Nyambita alishukuru kwa fursa hii ya ukubali wa uongozi wa hospitali ya Shirati kuahidi kwamba wakiwa na nafasi wakati mwingine watafanya mengine zaidi na zaidi na wito ukitolewa kwa wadau wengine pia kufanya jambo kama hili sehemu zingine zilizo na mahitaji.
Hawa ni waimbaji wa Born to Praise walipokuwa kwenye kushiriki tukio la huduma kwa hospitali ya Shirati jana.
Hawa ni waimbaji wa Born to Praise walipokuwa kwenye kushiriki tukio la huduma kwa hospitali ya Shirati jana.



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA