Sunday, September 18, 2016

Takribani siku 22 zimepita sasa tangu kuwepo na tukio kubwa la IMBA KWA AKILI lililokuwa limesheheni mibaraka ya aina yake kwani waimbaji na wadau wa nyimbo za injili toka sehemu mbalimbali walikusanyika katika fukwe za Msasani kushuhudia kilichokuwa kimeandaliwa.
Ikiwa bado ni msimu wa kwanza, IMBA KWA AKILI ikiongozwa na mratibu wake Martin Ngussa inaendelea vyema kwani mapema leo kumekuwa na zoezi la wimbo walioweza jifunza wanakwaya hawa siku ya tukio hilo Agosti 28, 2016 katika viwanja vya Msasani beach Dar Es Salaam wimbo unaitwa Ayubu. Zoezi la leo lilikuwa maalum kwa ajili ya mandalizi ya mwisho ya kurekodi audio hiyo ambayo itarekodiwa na studio za Ligo na kisha video kufanywa na Msanii Records na walimu wa zoezi la leo walikuwa ni Martin Ngussa, Elisha Ngussa na Clement Makubi.


Picha zote na Elisha Ngussa
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA