Sunday, September 18, 2016

"Yesu hakuwahi kujizuia kutamka neno moja la kweli, bali daima alilitamka kwa upendo. Alitumia uangalifu na tafakari kubwa katika kuchangmana na watu. Kamwe hakuwa jeuri, kamwe hakutamka neno la kuudhi bila sababu yoyote, kamwe hakuwahi kusababisha maumivu yasiyohitajika kwa roho inayoumia. Hakuwahi kulaumu udhaifu wa kibinadamu. Alisema ukweli, lakini daima katika hali ya upendo. Alikemea hali ya unafiki, hali ya kutoamini, na hali ya uovu: lakini machozi yalikuwa kwenye sauti yake alipokuwa akiyatoa makemeo yake makali. Alililia Yerusalemu, jiji alilolipenda, ambalo lilimkataa Yeye aliye njia, na kweli, na uzima. Maisha yake yalikuwa ya kujikana nafsi na ya kuwajali wengine. Kila roho ilikuwa ya thamani machoni pake. Pamoja na kudumisha hadhi yake ya Uungu, bado aliinama chini kumfikia kwa unyenyekevu kila aliye kwenye familia ya Mungu. Katika kila binadamu aliona roho iliyoanguka ambayo ilikuwa wajibu wake kuiokoa." (Steps to Christ uk. 12)


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA