Friday, September 23, 2016

Jaji wa mahakama kuu jaji David Maraga ndio jaji mkuu mpya wa Kenya
 Katika moja ya habari zilizofika injilileo Blog ilikuwa ni hii pale alipokuwa bado ni hakimu akiwania nafasi hii, Mr Maraga alisema itakuwa ngumu kwake kufanya kazi ya kesi siku ya Sabato na kwani siku hiyo ni pekee kwa kumwabudu Mungu na hakuna kazi itakayomfanya kumwacha Mungu wake, siku hiyo pia hataweza kwenda kanisani isipokuwa amekufa au akisaidia mtu katika ajali, aliyasema hayo mbele ya kamati ya mahakama iliyokuwa ikifanya mahojiano kwa wagombea wa nafasi hiyo.

 HATIMAE ACHUKUA NAFASI YA UJAJI MKUU.......
David Maraga atachukua mahala pake Jaji mkuu mstaafu Willy Mutunga ambaye mda wake wa kuhudumu ulikamilika iwapo ataidhinishwa.Jina lake litawasilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta ili kuidhinishwa rasmi kabla ya kuwasilishwa mbele ya bunge ili kujadiliwa na kupitishwa.
Maraga mwenye umri wa miaka 64 aliwashinda wenzake 13 ambao pia walituma maombi yao ya kugombea wadhfa huo wa juu,akiwemo jaji wa mahakama ya juu Jacton Ojwang na Smokin Wanjala ,msomi Makau Mutua miongoni mwa wengine.
Majaji hustaafu wakiwa na umri wa miaka 70 hatua inayoaaminisha kwamba Maraga atahudumu kwa miaka sita.
Habari/Picha na BBCSWAHILI

  HAPA  JAJI ALISEMA MACHACHE MARA TUU BAADA YA KUCHAGULIWA
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA