Wednesday, October 05, 2016

Ev. Eliezer Mwangosi
Luka 19:5 "Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako".

Pamoja na mafundisho mengi tunayoyapata kutoka kisa cha Yesu na Zakayo, somo la leo linatuhakikishia kuwa Yesu ametuona, na ameona haja za moyo wako. Haijalishi una hali gani, na watu wanakuonaje, maadamu ndani ya moyo wako wako umeamua kwa dhati kukutana naye.

Zakayo alitamani sana kumuona Yesu ili apate kuutua mzigo wa moyo wake, baada ya kusikia na kuguswa na Upendo wa Mwokozi. Japo alikuwa mfupi, ukiongezea tabia yake ya dhuluma, watu hawakuwa tayari kumpisha ili akutane na Yesu. Ndipo akaamua kupanda juu ya Mkuyu ili amuone huyu mtu wa pekee aliyejaa sifa za Upendo wa ajabu. Ndipo Yesu akamuona na Kusema "Shuka chini, leo imenipasa kushinda nyumbani mwako".

Makutano wakaanza kunung'unika wakisema "Ameingia kukaa kwa mwenye Dhambi", ndipo Yesu akamwambia "Leo wokovu umefika nyumbani humu ... Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea" Luka 19:6-10. Zakayo akapata nafasi ya kuokolewa, japo kulikuwa na vikwazo vingi na kuelemewa na mizigo ya Dhambi.

Rafiki; haijalishi una hali gani ya kutofaa kwa namna yoyote ile, iwe ni dhambi kubwa kiasi gani, hata watu wengine, na hata wewe mwenyewe ukajiona hufai, inawezekana watu wamefikia kukubeza, na wakati mwingine kukudharau, YESU anasema wokovu umefika nyumbani mwako leo.
Kumbuka Yesu alikuja kutafuta na kuokoa wenye dhambi. Simama kwa ujasiri, sikia sauti ya Yesu, SHUKA CHINI, nyenyekea chini ya msalaba .... Yupo hapa leo kwa ajili ya waliolemewa na kukata tamaa. Hakuna Dhambi kubwa wala changamoto yoyote inayoishinda NEEMA YA MUNGU, tambua huu ni wakati uliokubalika kwako, mtazame Kristo Akushindie.

WEMA WA MUNGU UKAWE JUU YAKO DAIMA

NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.


Na: Ev. Eliezer Mwangosi  - Tel. 0767 210 299.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA