Halikuwa kusudi lake Kristo kubadili, kuondoa, kutangua,
wala kuibatilisha sehemu yo yote ya sheria hii. "Msidhani ya
kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja
kutangua, bali kutimiliza." (Mathayo 5:l7).
Badala ya kuitolea sheria hiyo sifa mbaya, Kristo alikuja kuifanya iadhimishwe. "BWANA
akapendezwa kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria na kuiadhimisha." (Isaya 42:21).
Naam,
kwa kadiri Sabato inavyohusika, Kristo aliitunza, pamoja na kila amri
nyingineyo. "Siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa
desturi yake." (Luka 4:l6).
Kusema
kweli, imani kwa Kristo, badala ya kuiweka sheria kando, inaithibitisha
na kuiimarisha. "Basi, je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo?
Hasha! kinyume cha hayo twaithibitisha sheria." (Warumi 3:3l).
Sheria
hii ya Mungu, ambayo ndani yake imo amri ya Sabato, inatangazwa na
Paulo kuwa ni "ya rohoni," "takatifu," "ya haki," na "njema."
"Kwa maana twajua ya kuwa torati [sheria] asili yake ni ya rohoni"
(Warumi 7:l4). "Basi torati [sheria] ni takatifu, na ile
amri ni takatifu, na ya haki, na njema." (Warumi 7:l2).
Sheria
hii ni lazima ishikwe kama sharti la kupata uzima wa milele. "Heri
wale wazishikao amri zake, wawe na haki kuuendea huo mti wa uzima, na
kuingia mjini kwa milango yake." (Ufunuo
22:l4, Tafsiri ya King James Version).
Naam,
hiyo ndiyo kanuni, au kipimo, ambayo kwayo ulimwengu wote
utahukumiwa. "Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa
sheria ya uhuru." (Yakobo 2:l2).
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment