Sunday, December 25, 2016


 Mathayo 24:24-25 "Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele".

Kama kuna jambo la hatari ambalo Kristo aliliona juu ya watu wake, ni hila za shetani kuuteka ulimwengu wote hadi kuwayumbisha watoto wake Kwa kutumia Ishara, maajabu au miujiza akiwatumia makristo na manabii wa uongo. Wakati tunaoishi ni wa hatari kuliko Wakati mwingine uliowahi kupita, kwa sababu tayari wengi tumezaliwa katika kipindi cha kutimiza unabii.

Anachokifanya shetani kuwanasa wengi; anawatupia watu mishale ya matatizo mfano, magonjwa ya Kila namna yakiwemo, upofu, ukiwete, utasa, homa zisizoisha, UTI, ukichaa, ugonjwa wa matumbo n.k., ugomvi na kuvunja mahusiano au ndoa, mikosi na laana mbalimbali n.k. Matatizo yote yanayoletwa na roho chafu au roho za mashetani, mara nyingi hayaponi kwa dawa za kawaida yaani dawa za hospitali.

Kwa njia za roho za utambuzi, ambazo zinajigawa zingine kwa waganga wa kienyeji au waaguzi na zingine zinawaendea watu wa dini. Hivyo wapagani wanapoenda kwa waganga, wanaambiwa shida zao na roho zilizosababisha matatizo zinaondoka na mtu anakuwa mzima, ila huyo mtu anakuwa katika himaya ya mashetani, make ndiko alikopata tiba yake.

Kwa watu wa dini, shetani anawatumia watu wasiopenda kusimama katika kweli, anawajaza nguvu ya roho bandia, na kuwapatia roho za utambuzi, wakijua Kila chanzo cha matatizo ya watu, ambayo shetani amewaletea, na kwa kutumia biblia na jina la Yesu, wanayaondoa magonjwa kwa namna ya miujiza, Wakati ni shetani mwenyewe, aliyaweka na kuyaondoa, ndipo wengi wakishuhudia huamini kuwa kweli huyu ni nabii wa Mungu, hivyo hata akiwa anafanya UOVU, watu bado wanaamini ni mtumishi.

Katika kipindi hiki cha NEEMA, kila mtu ana uhuru wa kufanya lolote analo ona linampendeza, bila kufanywa lolote, wengi wanachukuliwa mateka na kuangamia kwa kukosa maarifa, falsafa nyingi juu ya kweli za biblia zimetungwa kuwapoteza wengi, wakitumia Ishara na miujiza. Watu wengi leo wanajenga Imani zao katika Miujiza waliyotendewa, hata wakiona wako kinyume na ukweli wa biblia wanasita kufanya matengenezo. Hiyo ndiyo hatari aliyoiona Yesu Kristo.

Zingatia; pamoja na utitiri wa manabii na watumishi feki, bado kuna manabii na watumishi wa kweli, hivyo tunachopaswa kukifanya ni kuwapima kwa neno la Mungu. Ukiona nabii anakataa wokovu kwa Imani katika Kristo sawa na Injili ya Yesu, au kama hafundishi watu Amri za Mungu (Kutoka 20: 3-17) kwa usahihi huyo hajatumwa na Mungu, sio kati ya watakatifu kwa mujibu wa biblia - Soma na kutafakari mafungu haya: Ufunuo 12:17, 14:12,  1Yohana 2:4, Isaya 24:4-6, Marko 7:6-9, Mathayo 5:17-20.

WITO: Yesu anatoa wito wa mwisho, kwa watu wote kufanya matengenezo, hebu kila mmoja watu auhakikishe wokovu wake kwa kutii neno la Mungu chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Usalama wetu ni kujisalimisha kwa Kristo, haijalishi unapitia changamoto zipi, au umejeruhiwa kiasi gani, bado Mungu anaweza kukutoa katika hali unayoipitia.

NAWATAKIA WOTE BARAKA ZA BWANA HASA TUNAPOFIKA MWISHO WA MWAKA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu 0767 210 299.
Soma na kuutafakari ujumbe huu halafu wapelekee wengine.





****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA