Tuesday, January 31, 2017


Waimbaji wa kikundi cha Yu hai
KUANZISHWA KWA KIKUNDI:
  Kikundi cha yu hai kilianzishwa rasmi mnamo tarehe 25/08/2013 katika shule ya Pugu sekondari   kikiwa na waimbaji watano, ambao ni Godson  Athumani sauti ya nne, Severine   Mlungwana sauti ya nne, Paul Elias sauti ya tatu, Yoel E. ndegea sauti ya pili na Enock Zabron sauti ya kwanza
JINA LA KIKUNDI:
  Tarehe 25/08/2013 ndipo jina la kikundi lilipatikana ‘YU HAI’ kutoka katika majina matatu ambayo yalikuwa yamependekezwa, majina hayo ni  sauti ya uamsho, nyota ya asubuhi na yu hai  ambalo ndilo lilipitishwa. Hakika MUNGU mwenyewe alichagua jina hilo, baada ya hoja nyingi kuhusu majina yaliyokuwa yamependekezwa, tulipiga magoti na kuomba ili MUNGU mwenyewe achague, mwenyekiti Godson alifumba macho baada ya ombi lile na kuchukua karatasi mojawapo kwa imani kuwa jina hilo ndilo litakalotumika maana MUNGU amelikubali. Hapo ndipo jina la kikundi lilipoanza kutumika rasmi.  Jina la BWANA LITUKUZWE.
Inaendeleaa..........

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA