Thursday, February 02, 2017


 Na Mchungaji James Machage
Kuhubiri ni njia ya kweli au wakala wa Mungu aliyechaguliwa kwa kufikisha ukweli kwa wanadamu. Mungu kupitia Mwana wake Yesu Kristo alitumia njia mbalimbali za kulihifadhi neno Takatifu yaani Biblia na kwa wakati wake likaanza kuhubiriwa toka mwanadamu mmoja kwenda mwingine.
Hali ya maisha ya sasa kuhubiri kunahitajika sana kwani ndilo agizo toka Bwana wetu (Math 28:19-20).

 Unapoanza kuhubiri kuna mambo ya kuzingatia;-
1. Unatakiwa uangalie hali ya ulimwengu kwa sasa mfano vita, uchumi, maadili n.k kuanzia hapo unaweza andaa somo lako.
2. Unaangalie mahitaji ya jamii husika
3. Ujiangalie wewe mwenyewe na hasa unapotoa visa 
4. Uinjilisti
  • ➠Mafundisho yahusu uinjilisti
  • ➠Yalenge mafundisho makuu mfano Mungu, Utatu mtakatifu, Neno la Mungu, Marejeo ya Yesu kwa mara ya pili n.k
  • ➠Maadili katika jamii, maana, umuhimu wake na ushauri juu ya maadili kwa jamii
5. Unapoandaa masomo basi yawe kwa namna yako mwenyewe wala sio kwa muiga mtu na njia za masomo hutofautiana kulingana na maandilizi kuwa tofauti.
6. Anza somo kwa ombi
7. Jisomee Biblia na vitabu vingine kama vya roho ya unabii na vitabu vingine rejea na uandae kwa tafakari.
Bwana akubariki unapopanga kurihubiri neno lake.
Mwisho.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA