Thursday, January 26, 2017

Mch. Christopher Ungani, katika eneo la ujenzi shuleni hapo
Kanisa la Waadventista wa Sabato, Nyanda za juu kusini linaendela na zoezi kubwa la ukarabati, na upanuaji wa miundo mbinu katika shule ya Sekondari ya Iringa.


Katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na mkurugenzi wa Mawasiliano wa STUM Mchungaji Ungani, ilishuhudia zoezi la ujenzi likiendela kwa kasi huku washiriki kutoka Mkoa wa Njombe wakiwa wameweka kambi kujenga majengo mawili ya Bweni la Wavulana huku Bweni la Wasichana likiwa limekamilika. 

Uboreshaji wa miundombinu ya Elimu imekuwa agenda kuu ya uongozi wa Konferensi chini ya Mwenyekiti Mch Kenan Mwasomola. 

Credit: Mjoli Edward Mazara

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA