Tuesday, January 03, 2017

1Petro 5:6-7 "Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu."

Nilikuwa nikipitia salaam za mwaka mpya, karibia wote walitakiana KHERI, yaani meema. Ni kawaida kila mwaka unapoisha na kuanza mwaka mpya kutakiana mema, lakini kiuhalisia wengi wanakiri mambo yanabaki vilevile, japo kwa wengine yanaweza kuwa mabaya zaidi au mazuri.

Hebu jaribu kuangalia, maisha ya tarehe 31 Desemba 2016 na hali ya maisha baada ya kuanza 2017; je ni tofauti? watu wengi mifuko imepwaya zaidi, huku wenye nyumba wakidai kodi, bila kusahau ada za shule na mahitaji ya watotot n.k. Heri ya mwaka mpya imeishia wapi? mbona mwaka unaanza na pasua kichwa?

Hata hivyo, wengi wakikumbuka mapito ya mwaka 2016, wanakiri, kama si Mungu, wasingefika salama 2017, ingawa kuna waliopita kwa machungu, wapo pia walioishi kama wako peponi, hata hivyo wote tunamshukuru Mungu tumevuka.

Neno la leo linatukumbusha jambo muhimu na la busara sana, kusalimisha maisha yetu kwa Mungu, ambaye hujishughulisha sana na mambo yetu, ingawa wengi hawajui, kumbuka; uhai tulio nao, afya zetu na mali zote, mwenye maamuzi ya mwisho ni Mungu. Na kadiri tunavyosogea mwisho wa nyakati, maisha bila Mungu ni sawa na kujilisha upepo.

Bila kujali uliyoyapitia mwaka jana au yanayoendelea, yawe ni majeraha au maumivu ya mahusiano, ya ndoa, ya ukata wa fedha, ya kukosa ajira, ya kunyanyaswa, ya kuporwa mume au mke, ya biashara, ya magonjwa sugu, ya mikosi na laana na kila aina ya fadhaa ... Mungu anasema mtwikeni yeye.

Mwaka 2017, unaweza tu kuwa tofauti na 2016, pale tutakapoamua kubadili mtazamo juu ya ahadi za Mungu, ambaye ndiye tu awezae yote, na kutazama upya mipango ya maisha, chini ya uongozi wa Mungu. Tukisalimisha maisha yetu na mipango yetu kwa Mungu, tutakuwa salaama, au laa shetani ataendelea kujeruhi na kutesa wengi.

NAWATAKIA BARAKA TELE MNAPOANZA MWAKA NA BWANA

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299 - Ya WhatsApp: 0766 992 265.




****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA