Tuesday, January 03, 2017


 Na Catheline Masiko
Mungu hajakosea kukuumba hivyo ulivyo,
Kwanini umkosoe? Kwani Mungu anakosea?

Hivyo ulivyo wewe ni mzuri dear hakuna wa kufanana na wewe kabisa jiamini!
Tafsiri ya mrembo ni kuwa halisia, sio MTU kuanzia kichwan hadi miguuni ni made in China tu then unaambiwa "woow umependeza" basi unafuraaaaahii mwenyewe, sikia rafiki
Mungu alkupa rangi nzuri nyeusi lakini wewe unataka kuwa mzungu hayo ni machukizo!
Hicho kipiriri Mungu alichokupa aliona unapendeza kuwa hivyo kinakufaa! Usibadilishe nywele kuwa za kizungu wale walizaliwa nazo, usiunganishe nywele yani (marasta, mawig n.k)
Nyusi alizokupa Mungu kama si nyeusi usizilamishe ziwe nyeusi kwa kupaka wanja au kuchora hina, unamkosoa Mungu!
Mungu alikupa kope zinazokutosha wewe, unataka kuziongeza kwa kubandika nyingine juu yake, ni machukizo
Masikio na Pua nzuri Mungu alikupa haina tobo, wewe unaamua kuitoboa ukifikiri Mungu labda alisahau, ni machukizo mbele zake.
Mdomo ulipewa mzuri, unaamua kupaka marangi ya ajabu ajabu pinki purple red hivi unajua chimbuko na tafsiri ya kupaka rangi mdomoni? Unajua maana yake kweli? Ni machukizo hayo rafiki
Mungu alikupa kucha nzuri nyeupe safi kabisa, wewe unasema dah Mungu ungemalizia kabisa na kupaka rangi unaamua kuipaka kila style, ni machukizo hayo!
Kifua Mungu alikupa cha kukutosha, wewe unasema aah ngoja nipunguze/niongeze kidogo, unaamua kupunguza/kuongeza matiti kwanini? Hujiamini au? Unamchukiza Mungu
Hips na makalio Mungu alikupa ya kukutosha kwa kadri alivyoona inakufaa, wewe unasema aah Mungu umenipa kidogo unaamua kuongeza , hakika hasira ya Mungu itawaka juu yako
Mwili wako ni Mali yake, unautoboa, unachora tatoo , unaupa makorokocho korokocho kwanini? Mmiliki amekuruhusu kufanya hivyo?
Watu waliokua wanafanya hayo hapo juu walijulikana kama makahaba, sasa wewe unaefanya hayo Leo tukuite Nani?
Tubadilike, tusipobadilika hakika Jehanam yatungoja kwa kumkosoa Mfalme mkuu, Bwana wa majeshi, Mungu Yehova!
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA