1Yohana 4:7-8
"Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila
apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa,
hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Kati
ya mambo ambayo shetani ameyatumia vibaya ili kuwanasa, na kuwajeruhi
wengi ni neno UPENDO. Shetani ameharibu akili za vijana na wazee kwa
kutumia neno hili upendo, wengi wameshindwa kujua tofauti kati ya upendo
wa kweeli na tamaa ya macho au mwili. Mtu akiambiwa NAKUPENDA, nati
zote za mwili zinalegea, bila hata kujua nini kinafuata.
Wengi
wamepitia maumivu yasiyoisha, hadi kufikia kujijutia nafsi, kwa sababu
tu ya kuukubali upendo feki wa tamaa za ngono, uliokuja kama upendo wa
kweli. Vijana wengi wanaanzisha uchumba wa kichina (Feki), na unaishia
kwa kuumizana, bila kusahau ndoa zinazogeuka ndoano, yote ni kwa sababu
ya kutojua maana sahihi ya Upendo unaoanzisha mahusiano.
Utasikia
kijana anasema; "Naamini hunipendi" eti sababu kakataliwa Ngono. Hivyo
tafsiri ya shetani ya neno Upendo au kupenda kwa watu wa jinsia tofauti
ni kutimiza tamaa za Mahaba au kudunguana maembe, wakati tafsiri ya
Mungu ni kutii AMRI za Mungu ikiwemo ya "USIZINI" au kuwa na tabia ya
Mungu - 2Yohana 1:6.
Hebu kila mmoja
ajihoji, ni upendo gani uliowaunganisha? au ni upendo gani unaoendelea
kati yao? Nani anautawala, ni Mungu au yule mzee wa mkuzimu? Mahusiano
yako na huyo unayemwita sweteee au mchumba au hawala, boy friend, babeee
au yeyote unayeishi naye na kufanya naye ngono, NJE AU KABLA YA NDOA
HALALI, unafikiri mwisho wake ni upi? Usidanganyike huo ni mtego na
umeshanasa.
Bado mlango wa wokovu wa kweli
ungali wazi, vijana kwa wazee wanaalikwa kuingia, kwa maana usiku
umeendelea sana na pambazuko la kheri liko karibu. Bado tumaini la
kumshinda shetani lipo kwa wote wanaosalimisha maisha yao kwa Mwokozi.
Mtajeruhiwa
na muovu shetani hata lini? kujiita, mkristo, nimeokoka, mpendwa, mcha
Mungu, mwimbaji, nambii, mtumishi na kuhudhuria kila huduma za ibada na
maombi, havina maana kama mkuu wa giza ndiye anayetawala maisha.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA WEMA WA MUNGU
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Mawasiliano: 0767 210 299 - WhatsApp - 0766 99 22 65
Utabarikiwa ukiwasambazia wengine ujumbe huu.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment