Monday, February 13, 2017







MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.

MAFUNGU: 1 Samwel 28:6,7; 1Samwel 8 :6,7,10,18,19; 1Samwel 16:1-2
“Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye BWANAhatawajibu.”(1 Samwel 8:19)

Je umewahi kutafuta kuijua sababu ya Mungu kutojibu maombi au unaongeza tu kuomba? Kumbuka maombi siyo yanayomsukuma Mungu kujibu ila imani yetu. Je unaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu au unaomba kutokana na tamaa yako?
Mungu si kama jini unaloliita kukutimizia lolote unalotaka. Mungu hajibu maombi yanayopingana na mapenzi, au matakwa yake yanayopatikana katika Biblia.
Inawezeka na wewe umeombea hitaji lako kwa muda mrefu na huoni majibu, umetubu DHAMBI,Nakwambia sababu ya kutokujibiwa ulichokuwa unaomba utendewe hakikuwa mpango wa Mungu lakini MUNGU atabaki kuwa MUNGU jifunze kurudi kwa Mungu kumuuliza usilalamike.

Mtumishi wa Mungu-Sauli,alikuwa kwenye shida, na akaenda mbele za Mungu kumuomba amsaidie, lakini Biblia inasema Mungu akakaa kimya, Baada ya kuona Mungu hamjibu,akageukia pepo.Dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone,hata hataki kusikia.Bwana anasema tukitafuta njia yetu wenyewe BWANA HATA SIKIA
Iko neema ya kutosha kwani katika mafanikio yako,taabu yako elewa kuna mtu/watu wanakuombea. BWANA ana hitaji watu jasiri wa kuikataa dhambi,shujaa wa Bwana Daudi mwana wa Yese. Hatutakiwi kushindwa; Tafuta nguvu ya Mungu kutosha kuleta ushindi! Amen
Habari kwa hisani ya Kirumba Seventh-day Adventist Church

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA