Monday, February 13, 2017



                                                          

Fikiria  juu ya michezo ya kama;
=Mpira wa aina zote na namna unavyochezwa
=Ulimbwende ambapo watu hushindanishwa wakiwa nusu uchi
=Miziki ambapo watu hucheza wakiwa na mavazi ya ajabu sanaaaa ama huimba nyimbo ambazo humghadhabisha MUNGU

            HISTORIA YA MPIRA:

Mpira ulianza mwaka 1863 mwezi 10, walikuwepo watu kadhaa waliotoka katika shule kadhaa uingereza na club chache zilizokuwapo hapo, wakawa wamewakilisha vikundi 11 na ndio wakakusanyika mwezi 10,1863 na kuanza kutunga sheria za kupatana za mchezo.

Hawa ndio waliosababisha kiundwe chama cha mpira ambacho kinaitwa FA (FOOTBALL ASSOCIATION) cha England mwaka huu 1863 ambao ni mwaka wa karibuni sana Baada ya Kristo.

USHABIKI WA MPIRA NI KUSHABIKIA SHETANI

Kama tulivyoona tafakari pale mwanzo, hivi wawezaje shabikia watu kufukuza mpira na ukawa na midadi na ushabiki wa juu kabisa hadi kufikia kujinyonga endapo Timu yako imefungwa pasipo misingi ya ushetani? “ Ni rahisi sana mtu kufa kwa ushabiki wa mpira wa miguu kuliko kufa kwa kumtetea Mungu wake”,

DONDOO KUDHIHIRISHA MPIRA NI MPANGO WA SHETANI

(i) Shetani kajiwekeza zaidi katika anasa/starehe na ambazo binadamu hupenda(Uzinzi,ulevi,mpira) ili kuwavuta wa wanadamu.Starehe za kidunia ni mali za shetani na anafanya hayo kurecruit wafuasi.Ni rahisi sana kukesha unaangalia mpira au mapambano ya ngumi kuliko kukesha ukiswali/kusali katika mkesha.Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mashabiki kuliko kutoa futari mwezi mtukufu.

(ii) (WAKOLOSAI 3:17) “KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI LOTE KWA JINA LA BWANA YESU NA KUMSHUKURU MUNGU BABA“Ni muhimu kuelewa ndani yetu tuliokoka kuna mafuta au tuna dhamiri ambayo inatufundisha kujua mema na mabaya (1PET2:26-27).Hata kama jambo hatujajifunza kwa undani juu ya jambo fulani,ndani yetu kutakuwepo roho mtakatifu akitufundisha kuwa hapa siyo na hapa ndiyo.


Sasa kila tunalolifanya kwa neno au kwa tendo, anasema tulifanye hayo yote kwa kufungua kwamaombi.sasa kutokan na mafuta ndani yetu JE TUNAWEZA KUFUNGUA MECHI YA MPIRA KWA KUSHUKURU BABA KWA MAOMBI? Utaona ndani yetu inakataa.

(iii) (YOHANA 5:19) “MWANA HAWEZI KUTENDA NENO MWENYEWE ISIPOKUWA AMEMUONA BABA ANALITENDA”. (YOH 14:6-9) Hivyo hatuna budi kujiuliza kutokana na maisha ya YESU, JE INAWEZEKANA YESU AKAWA ANACHEZA MPIRA? YESU KASHIKA MPIRA, MARA BEKi FULANI KAMKATA MTAMA AU TIMU YA YESU IMEPIGWA MAGOLI 6-0? kama dhamiri inakataa kuwa YESU hawezi kufanya hvyo na sisi hatuwezi kufanya hvyo.Tunatenda neno ambalo YESU anaweza kulitenda.

(iv) Asili au sifa za Mashabiki wengi wa jambo hilo, vinara wa jambo hilo , JE NI MATAIFA? Kama wanaongoza ni mataifa, basi nyuma ya jambo hilo kuna mashetani (UFUNUO 18:2-3,23) Mataifa yote yanapokuwa wanachukuliwa hivyo katika jambo hilo, ndio vinara, mashabiki, kwa namna hiyo hiyo uchawi unavyotajwa lazima tujue kuna roho za mashetani. Ukiona vinara au viongozi ndio waasherati au walevi, wavuta bangi. Hawa wanaotajwa washauri wa mambo ya kifundi katika timu hizo ndio wachawi wa timu.

(iv) Misingi ya mpira
Misingi ya ushetani pekee ndiyo inayo ufanya ushabiki wa mpira uwe na nguvu na kushangiliwa na mataifa.Ni rahisi sana kutoa ofa ya mpira kwa mshabiki na ukashangliwa kuliko kusaidia masikini wanaoteseka na adha ya dunia hii ukasifiwa huu mwezi mtukufu”.

Ni heri mtu Yule atoae sadaka na kufuturisha wanyonge kuliko anaetumia milioni za fedha kufadhili mpira kwa dk 90 tu .. Yamkini huenda ndiyo maana juzi ile timu ilifungwa chanzo kikawa ni hiki (washabiki kumradhi)

Kwa wale wanaokumbuka kisa cha mfalme suleimani hapo utagundua ndipo mpira siyo kusudi la Mungu;

(a). Ukisoma hiki kisa vizuri utagundua kile kisa cha mfalme suleiman na taranta za dhahabu 666 na zilivyopokwa na mpinga kristo, ambapo makombe ya dunia ya mpira yanaandaliwa kwa dhahabu.

(b). Ukiendelea kusoma vizuri utaona kuwa mfalme Suleimani akawa kaulaani upepo, na alisema pia pamoja na utajiri wote huu ni sawa na kujilisha upepo, hilo neno upepo, lilikuwa na maana ya bure kabisa, na baada ya hapo kilitengenezwa kitu mithili ya mpira kikajazwa upepo ili kudhihirisha u-bure huo usiofaa machoni pa Mungu... HUO UPEPO ndio unaojazwa mipira hadi leo na kukimbizwa kwa kulenga magoli.

(c). Kile kitufe mithili ya mpira chenye upepo, kilichezwa kwa kulenga katikati ya milingoti miwili mithili ya magoli na kushangiliwa na kerubi akiwa ndiyo mwamuzi (REFA).

(d). Wanafunzi wa yesu walikuwa 12, ukiondoa yule mmoja YUDA, walibaki 11 wenye Haki. Hao 11 ndio waliofungwa nira za kristo, lakini shetani hapo Kageuza, kwa kuweka wachezaji 11 katika team ya mpira, jiulize kwanini asingeweka 15? hao kumi na moja ndiyo wanaoshindana na kufungwa kwa mchezo wa kulenga ktk ya milingoti (magoli).

(e). Katika mchezo shetani ndipo alipouteka ulimwengu kwa kugeuza ahadi za Mungu.

Ukisoma bibilia Mungu kasema "Nitabariki kazi ya mkono yenu" lakini hapo shetani akageuza, wacheza mpira ndiyo wanaolipwa pesa ndefu zaidi kwa mda mfupi sana.. Maanake Hapo shetani aligeuza baraka za mikono kuwa za miguu (Agano la mapinduzi); Kama vile kule bustani ya edeni nyoka alivyogeuza.

(v) Clubs kubwa duniani, na waanzilishi wa hizo clubs na waendeshaji wa hizo clubs ni waabudu shetani(Devil worshipers) hata logo na majina  ya clubs zao ni za kishetani aghalabu;

(a) Manchester United (The Red Devils)
Ilianzishwa 1878 nchini England.Wanatumia rangi nyekundu na jina lake ni "Red Devils" yaani mashetani wekundu.Logo yao kuu ni kiumbe wa kipepo mf shetani/jini kashika uma wenye meno matatu  na juu ya kichwa chake kavaa crown  ya kifalme,maana yeye ndiye mungu/mfalme  wa Kuzimu & motoni

(b) Arsenal
Ilianzishwa jijini London mwaka 1886.Mmoja wa waanzilishi wake ni pamoja na Peter Healwood ambaye ambaye alikuwa ni  wanachama wa freemasons.Wanatumia alama ya silaha ya kivita (fataki) yenye magurudumu mawili kwaajiri ya kuisafirisha kutoka station moja mpaka nyingine.Hujiita"The Gunners".Ni kampuni ya waunda silaha za kivita/maangamizi.

(c) Chelsea (The blues)
"Chelsea" ni kampuni ya  pombe iliayonzishwa mwaka 1836 na ikazinduliwa  rasmi 14/3/1905.Wanajiita "the blues" kwa kadiri ya waabudu shetani hiyo ni blue satan kwa maana ktk lugha ya kiingereza hakuna wingi wa "blue",hivyo ile "s" humwakilisha shetani wa bluu aishiye moto usio na moshi(non luminous flame satan).Wana logo ya pepo/jini/shetani lililoshika na funguo za kuzimu(mamlaka za giza)

(d) Real Madrid (The white)
Ilianzishwa Hispania tarehe 06/03/1902
Wanatumia alama/Logo ya crown na inamaandishi " FMC" imetokana na kampuni ya kamali Bwin (Beat & Win)  ni kamali ni kinyume kabisa na mpango wa MUNGU.

Kwa haya tu machache ktk suala la mpira na baadhi tu ya clubs,kuna utukufu wa MUNGU  hapo?

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA