Sefania 3:17 "BWANA,
Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa
furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba."
Wakati watu wengi wanakosa matumaini na kuvunjika moyo kwa wanayoyapitia, neno la leo linatuongoza kuzitazama ahadi za Mungu kwetu. Tukitambua kuwa tuko vitani na ndani ya pambano lililofichika kati ya wema na ubaya, tunaweza kupitia hali zozote zilizo nje ya uwezo wetu, ikiwa ni machungu, huzuni, kujeruhiwa, kuonewa, kuvunjika moyo n.k. lakini bado yuko Mungu aliye juu ya yote.
Bila kujali unapitia hali gani kwa sasa, iwe ni baraka na furaha tele au vinginevyo, bila kumtumaini Mungu ni kujilisha upepo. Kama upepo usivyo na msimamo ndivyo yalivyo maisha ya mwanadamu, wewe ni shahidi, hata jana siku ambayo walimwengu waliita siku ya wapendanao (Valentine), bado kuna watu waliumizwa na waliowategemea kujirusha nao kwenye maraha, na wengine waliumia kwa kukosa hata wa kuwarushia maua hata kama ni ya mtandao, hayo yote bila Mungu ni upepo uvumao.
Neno la leo litusaidie kumsikiliza Mungu, na kuamini ahadi zake, tukidumu katika hayo, mioyo yetu itaponywa na kuokolewa milele, amani ya kimungu itaijaza mioyo yetu furaha daima. Upendo wake Mungu watosha kukidhi mahitaji yote ya mwanadamu, na hatimaye uzima wa milele. Huu ni wakati wa kila mmoja kumwabia Mungu "Kaa katikati yangu" ili nipite salaama na kupata tumaini katika ulimwengu usio na matumaini.
WEMA WA MUNGU UKAMZUNGUKE KILA MMOJA NA KUMPATIA MAFAIKIO TELE
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment