Friday, March 03, 2017


Kwa mila na desturi zetu tangu kale na kale tumezoea ni ngumu mdada kumwambia kijana anampenda
Njia rahisi hii hapa!
1.jitoe kwa Mungu kwanza,naye atakupatia hekima na maarifa ktk kufanikisha jambo hili,
RUTHU 3:1-3

2.Fanya urafiki naye kwa heshima msalimie kwa adabu wakati fulani anamzigo jaribu kumsaidia.
3.Jitahidi kuonana naye Mara kwa Mara aidha kazini,kanisani,-mtembelee lakini ziwe sehemu za wazi.
4.Jenga urafiki na rafiki yake kipenzi wa yule kijana,ambao utakuwa wenye nidhamu,pia au Dada wa kijana
5.Mtafute mama wa makamo ambaye ni wa heshima ;wanayeheshimiana na yule kijana,kisha jenga urafiki naye-mwisho uwe wazi kwa mama yule.
6.Mpende sana mama wa kijana na baba yake msalimie unapokutana naye,uwe radhi kumsaidia mzigo unapokutana naye.
7.Jiepushe sana kupayukapayuka mipango yako ni siri yako na Mungu ISAYA 41:21.
8.Mtumia kadi za pongezi kama birthday au ushindi wa jambo fulani, mtihani,cheo,kupata kazi,hata kama kazi ni ya Kanisa,ila usiandike neno lolote la mapenzi.
9.Toa zawadi ambazo si za bei kubwa,lakini ambayo ataithamini,kama ni msomi mnunulie Kitabu kizuri chenye ujumbe mzuri lakini isiwe Mara kwa Mara.
10.Tafiti kile anachopendelea,
11.Uwe na bidii. ya kazi.kama ni shamba Lima sana,kama ni ofisini wahi mapema,Acha mzaha kazini onyesha kujali muda wa kazi.
12.Panga kumsaidia kazi au wasaidie wazazi wake,kama unaishi nao karibu
13.Jifunze kupika chakula kizuri kisha siku moja umwalike,aje na rafiki yake,msiwe wawili peke yenu
14.Uwe msafi wakati wote,vaa nguo za heshima, uwe halisia usipende made in China
15.Jiepushe na marafiki walio na tabia mbaya asije akakuweka ktk kundi moja Amosi3:3
16.Jenga imani kwa Mungu,naye hatakuangusha kamwe.
Kwa hayo machache na mengine Mengi, kwa kijana mwenye nia ya kuoa #Atakuja_online_mwenyewe bila wewe kutamka neno ukaonekana mhuni au MTU wa bei rahisi rahis tu.
Barikiwa na Bwana
Na Catheline Masiko
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA