UGONJWA WA DENGUE (DENGUE FEVER)
Ugonjwa wa dengue ni mojawapo ya mgonjwa ya virusi yanayoenezwa na wadudu(ARBOVIRUS). Ugonjwa huu husababishwa na virusi wa dengue (dengue virus). Inakadiliwa kuwa zaidi ya watu milion 50 huugua ugonjwa huu kila mwaka duniani wakati watu wengine zaidi ya bilion 40 katika nchi 112 wakiwa kwenye hatari ya kupata maambukizi.Neno dengue inahisiwa kuwa lenye asili ya kiswalihi yaani ki denga pengo lenye maana aliyeshikwa na mapepo, hata hivyo ugonjwa huu umekuwepo tangu zamani katika historia ya binadamu. Kwa mujibu wa shirika la afya ulimweguni ugonjwa huu una enezwa na mbu kuliko magonjwa mengine ya virusi.
Kuna aina nne za virusi wa dengue. Maambukizi na aina moja hayawezi kumkinga mgonjwa kutopata aina nyingine ya virusi hawa. Hata mgonjwa aliyeugua aina moja akipata maambukizi ya aina nyingine hupata maradhi ya kuvuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili( DENGUE HAEMORRHAGIC FEVER).
Dalili za homa ya dengue
Wagonjwa wengi hupatwa na baridi na kujaa uso. Baadae mgonjwa huisi homa ,hutetemeka na hupata maumivu makali ya kichwa, mgongo na viungo. Homa hudumu kwa siku 2-7. na huweza kufikia nyuzi joto 41. Homa inayodumu zaidi ya siku 10 huenda haisababishwi na dengue.
Dalili nyingine zinazoambatana na maumivu ni:
.maumivu ya kichwa
.maumvivu ndani ya macho
.maumivu ya viungo
.kichefuchefu na kutapika
.vipele
.uchovu
.kukosa hamu ya chakula
.maumivu ya koo.
.kuvuja damu
.kuvimba mitoki.
Uchunguzi.
Uchunguzi unalenga kubaini virusi vya dengue kwenye mwili. Kipimo cha PCR hutumika katika utambuzi . Hata hivyo vipimo vingine hutumika ili kubaini kama mgonjwa ana maradhi mengine.
Matibabu.
Mara nyingi ugonjwa huu ukoma wenyewe bila matibabu yoyote.Hakuna dawa yoyote ya dhidi ya virusi hawa. Mgonjwa anashauriwa kunywa maji ya kutosha, kupumzika na kutumia dawa za kushusha homa kama paracetamol. Wagonjwa wanaopata tatizo la kuvuja damu wanahitaji uangalizi wa karibu hospitalini,
0 comments:
Post a Comment