Yale mahubiri yetu kwa njia ya Television ambayo yaliahirishwa wiki kadhaa zilizopita sasa yataanza rasmi siku ya Jumapili saa 9-10 STAR TV. Mahubiri hayo ni ya pekee sana na yametayarishwa kwa weledi wa hali ya juu ili kutofautisha na wale wenzetu.
Nimeambatanisa poster kama unaweza i-print na kuwasambazia watu. Tunatarajia wasabato wote watuunge mkono katika mradi huu mkubwa. Kama tulivyoaeleza hapo nyuma ni gharama sana kurusha vipindi hivi, lakini hatuna hofu kwani Mungu wetu ndiye mwenye fedha na dhahabu zote ulizonazo na alizonazo mwingine. Tumedhamiria kuendelea na vipindi hivi kwa wiki 28 ili mafundisho yote ya kanisa yapate kuwafikia watu kwa ukamilisfu.
Tunahitaji support yako kwa kualika marafiki zako kusikia habari hizi njema, na pia kusaidia fedha ili vipindi hivi visikwame. Kwenye hivyo vipindi tumeweka namba za simu kwa ajili ya kuchangia. Tuma m-pesa, tigo pesa ama airtel money, iwe ni 1,000, 2,000, 3,000, 10,000, 50,000, 500,000, 1,000,000 na kadhalika. Imani yetu ni kuwa pesa yako haitaenda bure, kwanza kuna mtu fulani ataokolewa na pili Mungu atakulipa.
[Namba zenywe ni hizi zifuatazo:
Tigo Pesa 0656 883317
M-Pesa 0757 402339
Airtel Money 0684 334416
KUANGALIA MAHUBIRI HAYA TEMBELEA PIA http://startvtz.com/
0 comments:
Post a Comment