Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa
Sabato katika Konferensi ya Mara Mchungaji Daudi Makoye amewataka watu
kuyashika maneno ya Mungu ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Kiongozi huyo ametoa agizo hilo mwishoni mwa
juma jijini Mwanza wakati akihutubia kwenye kilele cha mkutano wa Mkutano wa
Chama cha Wanataaluma na wajasiriamali Waadventista Wa Sabato
Tanzania (ATAPE) uliokuwa ukifanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini
humo ambao pia uliwahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi albino.
Katika mkutano huo ambapo
kulifanyika ibada ya kuwaombea watu wenye ulemavu wa ngozi
albino na taifa la Tanzania Mchungaji Makoye amesema jamii inatakiwa kuonyesha
juhudi ya kumweka Mungu mbele ili awe ngao na kinga katika maisha.
Amesema mtu yeyote asitegemee akili ya mtu
mwingine ili aweze kufanikiwa bali kila mmoja afanye kwa uwezo na akili yake
mwenyewe binafsi aliyopewa na Mungu na siyo kutegemea utajiri kutoka kwa viungo
vya albino.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ibada
hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arusha Dr Moses Muneja amewataka watu
wote kuwa na moyo wa huruma na kujitolea kutoa misaada yao inapohitajika bila
kujali kupata malipo.
Mkutano huo ambao ulikuwa wa kwanza
kuwahusisha watu wa rika na kada mbalimbali ulihudhuriwa na Mwakilishi wa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Sheikh Abdalah Hija na Mwenyekiti wa Kanisa la
Waadventista Wa Sabato wa Unioni ya Kaskazini Mwa Tanzania Dr Godwin Lekundayo.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment