Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika sehemu za kati,Mashariki,Kusini na magharibi mwa Tanzania.
KUTOKA TGF HADI KUZALIWA KWA E.T.F NA W.T.FBaraza kuu la union mwaka 1982 liligawanya TGF katika sehemu kubwa mbili,sehemu ya mashariki iliitwa EAST TANZANIA FIELD,mikoa yake ikawa ni 6 kwa Tanzania bara(Pwani,Dar Es Salaam,Morogoro,Dodoma,Lindi,Mtwara) na 5 kwa Tanzania Visiwani,yaani mikoa 2 Pemba na 3 Unguja.Makao makuu ya Fildi yakawa ni Misufini,Morogoro na kiongozi wa Fild yaani mwenyekiti akawa ni Mchungaji Zephania Bina.
Sehemu ya Magharibi iliitwa WEST TANZANIA FIELD.Mikoa yake ikawa ni 8 yaani Iringa,Mbeya,Ruvuma,Rukwa,Kigoma,Kagera Tabora na Singida.Makao ya fildi yakawa ni Iganzo Mbeya na Mwenyekiti wa Fildi akawa ni Mchungaji Elzaphan Wanjara.
Sababu ya mgawanyo huu ilikuwa kupunguza ukubwa wa maeneo hususani chini ya uongozi wa wazalendo ambao vyombo vya usafiri na Bajeti zao vilikuwa shida na hivyo jina la T.G.F.
MGAWANYIKO WA W.T.F
Fildi ya magharibi ilionekana kuwa bado ni kubwa kihuduma hasa ikihudumiwa kutokea Mbeya kwenda Bukoba na Karagwe.Mgawanyiko wa pili ulilazimika kufanyika tena mwaka 1991 ulioigawa WFT kama ifuatavyo;-Sehemu ya kusini mashariki ilipewa jina SOUTH WEST TANZANIA FIELD(SWTF)Mikoa yake ikawa ni Iringa,Mbeya,Ruvuma na Rukwa.
Sehemu ya Magharibi ikaitwa WEST TANZANIA FIELD Mikoa yake ikawa Kigoma,Tabora,Kagera,Singida na wilaya Mpanda.Makao makuu yakawa Mwanga,mjininKigoma,kiongozi wake wa kwanza akawa ni Mchungaji Msafiri Yohana.
ITAENDELEA JUMATANO.....
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment