HABARI KWA HISANI YA MTWARA SDA CHURCH BLOG(http://www.mtwarasda.org)
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0789 243 413 NA 0717 367 693***
Kanisa
la Waadventista Wasabato Mtwara limefanya ibada ya pekee kufungua mwaka
2015. Katika ibada hiyo, mchungaji wa mtaa wa Mtwara Pr. Zetti Ndola
amewaasa washiriki kujitoa katika kuifanya kazi ya Mungu mwaka huu.
Mchungaji Ndola amesema hakuna haja ya kukataa kushiriki katika kazi ya
Mungu pale tunapo hitajika kufanya hivyo.
Mchungaji
Ndola amewakumbusha waumini kuwa Mungu anao watendakazi wengi hivyo
usipo kubali kumtumikia mtu mwingine atachukua nafasi yako na hautapata
mbaraka.
Mara
baada ya hubiri la pekee Mchungaji Ndola alitoa wito kwa waumini
kujiweka wakfu na kujirekebisha pale walipo anguka mwaka uliopita.
Kwakweli Sabato ya leo ilikuwa ya pekee sana na Mungu amenena na wana na
binti zake kupitia mtumishi wake Mchungaji Zetti Ndola.
![]() |
| Waumini wakiwa tayari kwa huduma ya kuwekwa wakfu. |
![]() |
| Mchungaji Zetty Ndolla akitoa wito kwa waumini |
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0789 243 413 NA 0717 367 693***





0 comments:
Post a Comment