Saturday, February 07, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Gharib Bilal ameyasema hayo hapo jana katika  maazimisho ya miaka 5 ya utume Duniani kwa kanisa la waadventista wasabato ambayo yalikuwa na jina 'Uamsho na Matengenezo" na adhima kubwa ikiwa ni kusaidia waumini wa kanisa kujua wajibu wao kwa Mungu,kwa njia kutoa huduma kwa wahitaji hasa za afya kama kuchangia damu na kufariji waliokata tamaa kwa kusoma nao maneno ya matumaini kwa kuwapa kitabu cha 'Tumaini Kuu"
Kushoto ni Mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania wa kanisa la waadventista wasabato Mchungaji Magulilo Mwakalonge akiwa na mfasili wa siku hiyo Mchungaji Mussa Mika,Mchungaji Mwakalonge akitoa utambulisho kwa wageni na wenyeji waliofika ndani ya uwanja wa taifa,alimwambia Dkt Gharib Bilal kuwa japo uhuru wa dini upo lakini waumin wa kanisa hilo wamekuwa na changamoto ya kufukuzwa katika vituo vya kazi pia mashuleni kwasababu ya kutofika eneo la kazi siku ya jumamosi ambayo ni siku ya kuabudu kwa waumini hao.Aliendelea kwa kusema pia masharti na namna ya kupata viwanja au mahali pa kujengea sehemu za ibada yapunguzwe au kuondoka kabisa kwani huleta wakati mgumu wa waumini ambao huandaliwa kuwa raia wema katika nchi husika.
Kulia ni Sheikh al Hadi Musa Salim, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania akisema jambo hapo jana,Mchungaji Mwakalonge mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania ya kanisa la waadventista wasabato,Mke wa Dr.Blasious Ruguri na mwisho ni Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki ya kanisa la waadventista wasabato Dr.Blasious Ruguri ambaye ndiye mwenyeji wa shughuli zote hizi.
Askofu mkuu wa kanisa la Waadventista wasabato Dr.Mchungaji Ted Wilson akipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dr Jakaya Kikwete kwa kuzidi kulinda misingi ya amani na utulivu kwani kwa kufanya hivyo imefanikisha Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano hii ya utume (Mission Extravaganza)
Baada ya kusema jambo Dr.Ted alipata mda wa kusema jambo na Dr.Bilal
Dr.Bilal akitoa hotuba mbele ya waumini maelefu waliofika katika uwanja wa Taifa (hawapo pichani) mara baada kukaribishwa na Askofu mkuu wa kanisa la waadventista wasabato Dr Mchungaji Ted Wilson alisema serikali imejipanga kikamilifu kwa matukio makubwa ya uchaguzi mkuu na lile la kupigia kura katiba iliyopendekezwa.Aliendelea kusema kuwa uhuru wa dini utadumishwa kwa ungalizi wa serikali na akitoa ushauri kuwa kanisa lifanye hima kuwafundisha vijana juu ya adabu na utii kwa kuwapa mafunzo na namna ya kufanya kazi.Alijibu hotuba ya Mchungaji Mwakalonge kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itasaidia muda wote waumini wote kwani milango hilo ipo wazi,na tatizo la viwanja alisema serikali ataongea na mamlaka husika huku akimalizia kwa jambo la uhuru wa dini kuwa suala hilo litafanyiwa kazi.



Wanataaluma vijana wa kanisa wakipita mbele wa Mgeni Rasmi
Walimu na wanafunzi toka shule ya Sekondari Bupandagila wakipita mbele ya mgeni rasmi
Waandishi wa habari wakiwa kazini kuhakikisha kuna upatikanaji wa habari kwa tukio hili.
Waandishi wa habari wakiwa kazini kuhakikisha kuna upatikanaji wa habari kwa tukio hili.
Waumini wakifatilia tukio hilo

Viongozi wa vijana washupavu wa kanisa wakipita mbele ya mgeni rasmi na kutoa heshima mbele ya mgeni.
Kundi la wanawake toka Ukonga wakipita nao mbele ya mgeni rasmi.
Kundi la wainjilisti wa vitabu wakipita mbele ya Mgeni rasmi hapo jana.


Kundi la wanataaluma vijana wa kanisa la waadventista wasabato wakipita mbele ya mgeni rasmi.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA