![]() |
| Mchungaji Jonas Singo toka kanisa la Magomeni sda. |
Na Kamati ya Mawasiliano,Kirumba
WASHIRIKI wa Kanisa la Waadventista wa Sabato hapa nchini,wametakiwa kusimama imara katika njia moja ya kumfuata Mwokozi,kwa kuwa Mungu hapendezwi na watu Wasio na msimamo.
Mchungaji wa Mtaa wa Magomeni Jijini Dar es Salaam,Jonas Singo, amesema kuchelewa na kusita-sita kwa kutoamini kile anachosema Mungu,huwachosha Malaika wa Bwana wanaotuhudumiamaisha ya kila siku ili tupate wokovu.
Akizungumza katika hitimisho la Juma la Maombi ya Idara ya Wanaume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato(Adventist Men Organization) lililoanza Juni 12, Katika Kanisa la Kirumba,Jijini Mwanza,Mch. Singo amesema, washiriki wanapaswa kuacha kurejea nyuma walikotoka,mithili ya Waisraeli wa zama za Musa,waliochangamana na Wamisri walioshindwa kila mara kusonga mbele.
Amesema,washiriki wa sasa wameendekeza “MICHEPUKO YA KIROHO”,na kwamba sasa wakati umefika wa kubaki Njia Kuu, yaani kumfuata Kristo daima katika maisha yao yote.
Kauli hiyo imekuja,kufuatia tabia ya Ukristo wa leo kuchangamana na mila na desturi za Kidunia,kitu ambachoMchungaji Singo amefananisha na Safari ya Waisreli kutoka Utumwa wa miaka 400 Misri walivyochangamana na Wamisri wallioogopa Mapigo,maarufu kama “THE MIXED MULTITUDES” waliowashawishi Waisreli kurejea walikotoka.
Kauli Mbiu ya Maombi hayo ya AMO ilikuwa, “TUPATE UZOEFU WA KUTOKA” ikiwa na lengo la kuwaambia washiriki wa Kanisa kutoka katika mazoea ya Utumwa wa Dhambi,mithili ya Wana wa Israeli zama za Utumwa wa miaka 400.'
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***




0 comments:
Post a Comment