Mwanzo 2:18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe Peke yake, NITAMFANYIA MSAIDIZI WA KUFANANA NAYE".
Baada ya kutoa somo lililopita juu ya vijana na mahusiano, nimepata maswali mengi yanayoonyesha kuwa, vijana wamekabiliwa na JANGA KUBWA linalohitaji msaada. Maswali kwa mfano: Nisipo jaribu kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoa NITAJUAJE KAMA - Mwanaume ni Mzima? Binti anaweza mapenzi? Binti anaweza kushika Mimba? Binti ni Bikra? Atajuaje kuwa kweli nampenda? Umbile lake likoje?
Vijana! maswali yote hayo yapo kwa sababu 1.Akili zimekufa Ganzi haziwezi tena kuamini Ahadi za Mungu, Hakuna network na Mbingu, mawasiliano yamekatika kati ya Mungu na Vijana 2.Tamaa ya Mwili ndiyo inayo ongoza maamuzi ya akili. KUTOKANA na sababu hizo mbili, vijana asilimia kubwa bila kujali, wanajiita ni wakristo, wameokoka, ni wacha Mungu, ni Waimbaji nk. Wako chini ya Utawala wa Adui.
Kadri vijana wanavyotumia akili zao KUCHAGUA, KUONJA na KUACHA, ndivyo wanavyojitia katika Majanga ya kuwa na mabiti wengi wanaoharibu vizazi kwa kuchomoa mimba na kutozaa tena, kuwa na mabinti na wanaume walioharibiwa sifa za uaminifu, kuharibu maana ya UPENDO kuwa ni kukidhi TAMAA YA MWILI, vijana kuingia katika ndoa wakiwa na ladha tofauti ya Mapenzi jambo ambalo ni SUMU katika Ndoa itakayoanzishwa.
Kijana alivunja Ndoa wakiwa HONEY MOON, Baada ya kuambiwa "HAFANYI VIZURI KAMA WENZIE", swali lilikuwa wenzie akina nani? Ndivyo utasikia vijana wa kiume wakihadithiana juu ya ladha tofauti za mabinti, UCHAFU huo wa akili ukiingia kwenye Ndoa SUMU. Kuna Siri kubwa katika maumbile ya uzazi yaliyo tofauti kwa kila mtu kwa ajili ya kukidhi starehe ya Ndoa.
Matatizo ya kuvunjika uchumba yatazidi kuongezeka, kwa sababu mahusiano yanasalimishwa kwa SHETANI chini ya dhambi ya Uasherati, ndio maana utashangaa, mapenzi yanavunjika ghafla, kube umeendewa kwa Mganga umetupiwa NUKSI, mpezi Wako anakuona wa ajabuajabu tu, ukimuuliza vipi mbona sikuelewi naye anasema, hata mimi sielewi. Ahaaa, hayo ndiyo matokeo, ya kufanya Dhambi ya zinaa, Mungu amewaacha, shetani anashika usukani, utaishia kuoa zee au Binti mchawi au Binti usiyemtarajia, huko nje kuna wengi wanawinda bila kulala. BILA ULIZI WA MUNGU NI MAJANGA.
USALAMA; ni Mungu peke yake mwenye uwezo wa kukupatia atakaekidhi hitaji la Ndoa, atakupatia wa KUFANANA na wewe, hapo ndipo penye siri kubwa ambayo Shetani anaipiga vita, vijana wanaishia kubeba KOROMA wakidhani NAZI. Mungu hawezi kukupa Kitu Kibovu, mfano; akupatie Kijana asiyeweza tendo la Ndoa. Isipokuwa hali inaweza kutokea mkiwa ktk ndoa, kwa mfano; kutokana na magonjwa, hapo haina jinsi inabidi kumuomba Mungu awapatie kuvumiliana.
Kwa leo tuishie hapa, ila kuna mambo mengi mnayohitajika kusai diwa ili muweze kupita salama katika JANGA hili, ambalo wengine tayari ni wahanga wanaohitaji msaada wa dharura na wegine ndio wamesimama masikio juu wanaelekea kuzama, wangine Wako wanajiadaa kuingia.
MUNGU AWAJALIE HEKIMA YA MBINGUNI ILI MUWE NA MAISHA YENYE FURAHA DAIMA
Na. Ev. Eliezer Mwangosi, Tel. 0767210299, Email. Eliezer.mwangosi@yahoo.com
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment