Muimbaji wa nyimbo za injili aliyeamua kumtumikia Mungu kwa kutumia sauti yake Miriam Chirwa ametoa lake la moyoni pale aliposema anavutiwa sana na muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Angel Magoti.
Miriam aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na muandishi wetu walipokutana katika kanisa la Waadventista wasabato Kimara jijini Dar es Salaam alipoalikwa kutoa huduma ya uimbaji katika sabato ya wageni ya tarehe 21/06/2015.
Pia aliongeza anatamani ile sauti yake yote ingeshuka juu yake maana anavutiwa sana na huduma ya muimbaji mwenzake Angel Magoti. Injilileo ilipohitaji kufahamu kama alishawahi kumueleza Angel habari hiyo alisema hajawahi ila atafanya hivyo mapema nasi tulimuahidi tutaikisha ujumbe huo kwa Angel.
Zaidi aliomba akumbukwe katika maombi kwani Mungu amesikia maombi yake yale aliyokuwa akimuomba na siku sio nyingi ataondoka kwa ajili ya kwenda kuanza elimu yake ya Sekondari.
Injilileo Blog tunamuombea mafanikio katika mipango yake yote yeye pamoja na familia yake.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

| Miriam Chirwa akiimba katika sabato ya wageni Kimara |
Injilileo Blog tunamuombea mafanikio katika mipango yake yote yeye pamoja na familia yake.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment