| Mchungaji Mwakalindile mkurugenzi wa Redio ya Morning Star asubuhi ya leo akitoa mada juu ya mambo muhimu katika uletaji watu kwa Bwana kwa kutumia Redio pale tunapoandaa vipindi. |
| Mchungaji Mwakalindile mkurugenzi wa Redio ya Morning Star asubuhi ya leo akitoa mada juu ya mambo muhimu katika uletaji watu kwa Bwana kwa kutumia Redio pale tunapoandaa vipindi. |
| Pichani ni Mrs.Jullie Ochieng mkufunzi wa semina hizi toka nchini Kenya. |
| Mchungaji Mussa Mika ni moja ya wakarimani katika semina hizi.. |
| Mchungaji Steven Bina ni Mkurugenzi wa mawasiliano toka Divisheni akifatilia mkutano mapema leo ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato Arusha Mjini Kati. |
Idara ya Mawasiliano
ni kitu cha umuhimu sana katika maisha yetu hasa kwenye kipindi hiki,Mchungaji
Mwakalindile ameeleza muhimu wa vifaa vya Mawasiliano na teknolojia inapozidi
kuongezeka basi kuna kila haja ya kutumia kwa ukaribu sana vyombo vya mawasiliano
mfano mama Ellen G White alitumia teknolojia hii kwa kuchapisha magazeti ya unabii kwenye karne ya 19 na
akishauri kuwa siku za usoni njia za kipindi chake za Mawasiliano zisitumike kwenye kipindi
cha sasa tokana na teknolojia.
Kanuni
chache za ufanisi wakati wa uandaaji wa habari na kuwa mwanamawasiliano mzuri.1.Jenga mazoea ya kuongea vitu ambavyo unayafahamu vizuri na
kutumia muda wako vizuri kujiandaa na kusoma hasa kwenye uwasilishaji wa
habari.
2.Wafahamu
wadhira au watu unaowafikishia ujumbe na kuwa ni waina gani hasa kwenye vyombo
vya habari uku ukijua unasikilizwa na watu wa rika nan chi zote za Dunia tena
wakiwa kwenye aina tofauti tofauti za kipato.
3.Toa ujumbe
unaogusa mahitaji ya watu mfano kwa wana masoko na wafanya biashara kuona
mahitaji na changamoto zao na kuongea vitu vinavyowagusa watu
4.Unapoogea
na watu wafanye hadhira waone kama unaongea na mtu mmoja na tena kwa uchangamfu
na angalizo likiwa mahubiri yetu yawe yanayolingana na mahala tulipo na
kupunguza kelele kwani vifaa vya studio vinanguvu ya kunasa sauti.
Tv-unapoongea
kwenye tv ni muhimu pia kuwa makini kwa muktaza wa muonekano wako kama kuweka
kidole puani.
5.Zungumza
kwa kutumia maneno mazuri wala sio yanayouumiza kwa lugha nzuri ambayo sio ya
lazima ambayo yataleta picha nzuri kwa jamii ya vyombo vya habari ndio chachu
ya kuleta ujumbe huu wa tumaini.
6.Ni vizuri
yakaambatana na maandishi itasaidia kuongea kwa muda na mpangilio mzuri ukiwa
ndani ya Redio na ikipendekezwa kuwa mtu anayesikiliza atoe mrejesho wa kile
kinachohubiriwa.Na inaonekana pia mwanamawasiliano mzuri ni yule anayeweza
kusikiliza
7.Muda ni
kitu muhimu sana kwenye Mawasiliano na utunzaji wa muda
MULTMEDIA
COMMUNICATION
Ni bora Zaidi
kutumia njia nyingi za Mawasiliano kwa njia ya sauti na picha na hapa uwezo wa
kujibizana kwa mtumaji na mpokeaji ili kupeana jumbe na kushirikiana.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment