MILCA KAKETE –KATIKA UMRI MDOGO SANA ALIANZA KUIMBA KATIKA KWAYA KANISANI.
AKIWA SHULE YA MSINGI ALIINGIA
STUDIO KWA MARA YA KWANZA KAMA SOLOIST WA NYIMBO KADHAA NA KWAYA YA KANISA LAKE
KU NKINGA CHRISTIAN CHOIR(TABORA).
MNAMO MWAKA
1999 NA 2000 AKIWA NI KIONGOZI WA SIFA KATIKA KANISA LA PENTECOSTE KURASINI
ALIPELEKWA NA KANISA KUHUDHURIA SEMINA YA VIONGOZI WA SIFA NCHINI KENYA.
MWAKA 2003 MUNGU AKAONGEA NAYE KUTOA ALBUM YA KUABUDU INAYOITWA
“YESU NIKO MBELE ZAKO” INAYOBEBA WIMBO ULIOGUSA MIOYO YA WENGI NA KUPENDWA
“NATAMANI KUFANANA NAWE” “NIFINYANGE” PAMOJA NA “HERI NI JINA” AMBAO UMEKUWA
UKITUMIWA KATIKA RADIO KWA MAHUBIRI YA MTUMISHI WA MUNGU MWAKASEGE
KANDA HII ILIGUSA MIOYO YA WATU WENGI NA SI
KUGUSA PEKE YAKE BALI MUNGU ALIPONYA KUPITIA KANDA HII . MILCA ANASEMA “NILIPATA
USHUHUDA TOKA KWA MTU ALIYEPONYWA UKIMWI BAADA YA KUAMBIWA NA MUNGU AKIWA
CHUMBANI KWAKE KWAMBA ASIKILIZE KANDA ILE, KISHA KWA MUDA KAMA NUSU SAA ALIZIMIA NA
ALIPOZINDUKA AKASIKIA SAUTI IKISEMA MSHUKURU MUNGU MAANA UMEPONA! AKAENDA
KUPIMA ZAIDI YA MARA MOJA HAKUWA NA UKIMWI TENA-UTUKUFU NI WA MUNGU PEKE YAKE”.
SASA MILCA
KAKETE AMEKUJA NA ALBUM MPYA INAYOKWENDA KWA JINA “NAKUNG’ANG’ANIA” NA NYINGINE YA KUABUDU INAITWA “NATAKA
NIKUABUDU” ZIPO MADUKANI.
0 comments:
Post a Comment