1: Amini huyo mke/ mme umepewa na Bwana Mungu wako, ukaishi nae siku zote za maisha yako, umpende, umtunze, umlinde, umjali, umheshim, umthamini na hakuna mke/Mme mwingine zaidi ya huyo umtazame yeye peke yake.
2: Ndoa ambayo haina furaha inatokana na dunia (mkabidhini Bwana maisha yenu na family Yenu)
3: Kila mmoja apate muda wa kumuombea mwenzake
4: Mwendee Mungu mweleze shida zenu si wanadamu.....Isaya 9:6
5: Pendo lionekane kwa mme au mke kwa vitendo sio maneno, kama ilivyozoeleka I love u love u too ( onesha upendo kutoka moyoni)
6: mpende mme/ mke wako kiasi cha kufa ( Thamani yake usifanishwe na yeyote)
7: Matatizo ya Mme yawe ya mke na ya mke yawe ya mme mchukuliane udhaifu, maana mmekua mwili moja( mathayo 19:4,6)
8: Matatizo yataturiwe mapema na yasijirudie rudie ( kurudia rudia makosa Yale Yale kila Siku)
9: Usitoe siri za ndani ukapeleka nje 2 petro 2:13
10: Jifunze kutumia neno samahani na kujishusha pale ambapo umemkosea mwenzi wako na aliekosewa awe tayari kusamehe na kusahau Mathayo 18:21,22
Ukizingatia hayo na mengine unayojua ndoa yenu itakua ya Amani upendo na furaha siku zote na baraka za Bwana zitakua juu yenu
Tubarikiwe tunapopanga kufanya hivyo.....Amen
NA CATHELINE MASIKO
0 comments:
Post a Comment