Sunday, April 17, 2016



Maandiko yanasema kuwa baada ya rehema kufungwa kwa watu wote, Mungu atamwaga mapigo saba kwa waovu kabla ya Kristo kushuka toka mbinguni.
Nabii Danieli anasema:

kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lililopoanza kuwapo taifa hata wakati huo Danieli 12:1.
Injili ya milele itakuwa imehubiriwa kwa dunia yote. Wito wa kutoka katika mifumo ya ibada za uongo utakuwa umetoka,
Ukweli wa biblia umewekwa bayana na wanadamu watakuwa wamechagua kati ya amri za Mungu na amri za wanadamu.
Kazi ya Kristo kama Kuhani Mkuu mbinguni imemalizika. Kila kesi imeamriwa kwa ajili ya uzima wa milele au kwa ajili ya mauti ya milele. Kabla ya hawajachukuliwa mbinguni waaminifu watashuhudia mapigo makali ya Mungu kwa waovu.

                            MAPIGO SABA YA GHADHABU YA MUNGU
  • Imeandikwa (nukuu ni kutoka katika Biblia ya Kiswahili cha Kisasa)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, 'Nendeni mkamwage mabakuli hayo saba ya ghadhabu ya Mungu duniani
Ufunuo 16:1. Mapigo yataanguka moja baada ya jingine.

PIGO LA 1
  • Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama, na wale walioiabudu sanamu yake
Ufunuo 16:2. Kazi zote zitasimama na hospitali hali kadhalika kwa maana hata waganga na wauguzi ambao hawakusalimisha maisha yao watakuwa vitandani.
PIGO LA 2
  • Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini.
Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa
Ufunuo 16:3. Harufu ya kutisha, viumbe wa baharini watakufa.

PIGO LA 3
  • Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, navyo vikageuka damu
Ufunuo 16:4. Maji ya bomba na ya visima yatageuka kuwa damu badala ya maji. Hii itakuwa balaa kubwa.
PIGO LA 4
  • Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo: wala hawakutubu wala kumpa utukufu
Ufunuo 16:8,9.
PIGO LA 5
  • Na huyo malaika wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama ; ufalme wake ukatiwa giza: wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao , wala hawakuyatubia matendo yao na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao
Ufunuo 16:10, 11.
PIGO LA 6
  • Kisha malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Frati. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ilitengenezwa kwa ajili ya wafalme wa mashariki.
Kisha nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama, na kinywani mwa yule nabii wa uongo. Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza.
Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita kuu Siku ile ya Mungu Mwenye Uwezo Ufunuo 16:12-14.

PIGO LA 7
  • Kisha malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, Hekaluni, ikisema, Mwisho umefika! Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu. Visiwa vyote vikatoweka, nayo milima haikuonekena tena. Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno Ufunuo 16:17-18,20-21.
  • Uharibifu utakuwa ni mkubwa sana. Lakini Mungu atawalinda watu wake, kama alivyowalinda Israeli wakati wa mapigo 10 juu ya Misri
Kutoka 7-9
HITIMISHO
Kwa jinsi tunavyoishi sasa tunachagua upande gani tutakaokuwa aidha wa Mungu, au upande wa Shetani. Wakati mapigo haya yatakapokuwa yameanza watu watakuwa wamechelewa sana kubadili kambi! Mlango wa rehema utakuwa umefungwa tayari milele.! Ndipo wale waliokataa wito huu watakaposema; “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka” Yeremia 8:20. Wale waliong’ang’ania dini na imani za uongo za wazazi wao zilizobadili amri za Mungu, wakiwa wamechelewa watajua kuwa “… hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa” Yeremia 16:19. Mapigo haya yatakuwa ni kilele cha historia ya dunia hii unayoiona, na historia ya wote wapendao uasi. Hakika mwisho wao unatisha. Baada ya haya Yesu atashuka kuwachukua watu wake. Kwa nini rafiki yangu usijiunge na kambi ya Mungu sasa. Usisubiri, unapaswa kufanya maamuzi sahihi usije ukachelewa. Alama za nyakati zinaonyesha muda si mrefu Mungu atafunga mlango wa rehema zake.
BARIKIWA UNAPOMPOKEA YESU HILI UEPUKANE NA HAYA MAPIGO.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA