Saturday, June 11, 2016

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Kaskazi mwa Tanzania wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Mchungaji Dr. Godwin Lekundayo alitaka kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzani Kujiandaa kwa Mahubiri Makubwa yatakayo Fanyika Mwaka 2017 kwa wakati mmoja kwa Makanisa na  makundi yote Tanzania ili kuitikia kaulimbiu ya TMI(Total Membership Involvement )
Dr. Lekundayo Akirejea Mahubiri yaliyo isha hivi karibuni Huko Nchini Rwanda yaliyokuwa na Vituo 2300 na watu zaidi ya 97000 Kubatizwa alisema "Sisi Tanzania Kwasababu ya Ukubwa wa Nchi inatupasa kujipanga Mapema ili kubatiza watu zaidi ya Laki Mbili Kwa neema ya Mungu"
Mchungaji Dr. Lekundayo Amesisitiza kuwa Maandalizi yaanze Sasa yaani leo Tarehe 10/06/2016 ili kuwa na viwanja pia pesa za kusaidia wenye mahitaji na kadharika.
Amesema hayo Jioni hii katika Kipindi cha Kanisani leo Kutokea hapa Dodoma Katika Kanisa la Dodoma kati Mbele ya Wana TAiN wanao endelea na Mikutano yao inayo tegemewa kufungwa leo.
Ombea Mpango Huu Mkubwa ili BWANA ajipatie waliyo wake kwani sasa ni wakati Wa Mavuno. Amen
Habari / Picha na Haruni Kikiwa
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA