Tuesday, August 16, 2016

Katika mfululizo wa mafundisho yake kwa vijana ambao hawajaoa wala kuolewa, Uncle Chris alipata kufundisha namna vijana wa njinsia zote wanavyopaswa kuchukuliana mizigo kitabia na changamoto zote, kwani kwa kufanya hivyo wataweza kuishi kwa upendo katika mahusiano yao hadi watakapoingia kwenye ndoa.
Akibainisha tabia za njinsia ya kiume, Uncle Chriss alisema kuna baadhi ya wanaume ambao huwa sio wepesi kusema mapema kuwa wanahitaji kuingia kwenye mahusiano na msichana fulani na hivyo wanaishia tu kuumia, na kwa vijana wa kike hao ni vigumu sana kusamehe na hivyo vijana wa kiume wanapowaendea wanapaswa kuwa makini kwa yale wanayoyasema wasifanye makosa kwa kusema mambo yasiyo na maana."Ukishaona maneno kwake ni big issue jipange" alisema Uncle Chriss
Chriss Buhatwa





****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA