Somo la Asubuhi linatoka katika kitabu cha MARANATHA,
kitabu ambacho kinadhaminiwa na EGW Writtings maalumu kwa ajili ya
Programu ya IBADA.
Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia
kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha
kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 1 Yohana
2:18
Adui anajiandaa kwa ajili ya kampeni yake ya mwisho dhidi
ya kanisa. Amejificha sana asionekane na watu kiasi kwamba wengi
hawafikiri ya kwamba anaishi, na vivyo hivyo, wengi hawatambui shughuli
na ukubwa wa uwezo wake. . .
Mwanadamu ni mateka wa Shetani na kwa asili anafuata
mapendekezo na matashi yake. Ndani yake hakuna nguvu ya kupinga na
kuukataa uovu. Ni pale tu Kristo anapokuwa ndani yake kwa imani iliyo
hai...ambapo mwanadamu anaweza kudiriki kumkabili huyu adui mbaya sana.
Namna yoyote nyingine ya kujilinda haifai kabisa. Ni kupitia kwa Kristo
peke yake ndipo uwezo wa Shetani unazuiwa. Huu ni ukweli wa muhimu sana
ambao wote wanapaswa kuuelewa. Shetani anashughulika sana kila wakati,
akienda huku na kule, akipanda na kushuka duniani, akitafuta mtu ammeze.
Lakini ombi la dhati la imani litachanganya jitihada zake hata zile
zenye nguvu sana...
Shetani anategemea kuwahusisha masalio wa Mungu kwa ujumla
katika maangamizi yanayokuja katika dunia. Wakati kuja kwa Kristo
kunapokaribia, yeye (Shetani) atazidisha azma yake na uthabiti katika
jitihada ya kuwaangusha. Wanaume kwa wanawake watainuka wakidai kuwa na
nuru mpya au ufunuo mpya ambao kwa kawaida unavuruga imani ambayo
imekuwako katika misingi imara siku zote. Hata ingawa mafundisho yao
hayatakuwa na vithibitisho vya neno la Mungu, bado roho zitadanganywa.
Taarifa za uongo zitasambazwa, na baadhi watanaswa katika mtego huu...
Hatuwezi kuwa wazembe katika kuangalia aina yoyote ile ya makosa, kwani
Shetani anadumu kutafuta namna ya kuwavuta watu toka katika ukweli...
Wapo watu ambao hawako imara kitabia. Wako kama donge la
tope la udongo wa mfinyanzi ambalo laweza kuumbwa katika mwonekano
wowote. . . Udhaifu huu, kukosa maamuzi, kutokuwajibika, vyapaswa
vishindwe. Katika tabia ya kweli ya Ukristo ipo hali ya ujasiri usio wa
kawaida ambao hauwezi kutengenezwa au kushushwa hata hali iwe mbaya
kiasi gani. Watu wanapaswa kuwa na msimamo katika maadili, unyofu ambao
hauwezi kubezwa, kuhongwa au kutishwa. . .
Mungu ameweka mipaka ambayo Shetani hawezi kuipita. Imani
yetu iliyo takatifu sana ndiyo mipaka; na kama tutajijenga wenyewe zaidi
katika imani, basi tutakuwa salama katika utunzaji unaotoka kwa
Mwenyezi.****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment