Thursday, August 18, 2016

“Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazo farijiwa na Mungu.” (2 Kor. 1:3,4)
Je Paulo hutuambia nini kuhusu jinsi mateso yetu wenyewe yanaweza kutusaidia kuonyesha huruma na faraja kwa wale walio karibu nasi? Ni uzoefu gani umepitia kama (unao) ukweli wa maneno haya katika maisha yako mwenyewe?

Neno la kingereza “Comfort” limetoholewa kutoka katika lugha ya Kilatini,com ( yaani pamoja ) fortis( nguvu) kama Kristo hutuimarisha katika mateso yetu, tena hutuimarisha kupitia mateso yetu, tunaweza kupitisha nguvu hii kwa wengine, kama tulivyojifunza kutoka katika huzuni zetu wenyewe, tunaweza kwa ufanisi Zaidi kuwahudumia wengine katika matatizo yao.
Makanisa kwa ujumla wanawashiriki ambao wanakabiliwa na changamoto na wanao faraji , mchanganyiko huu unaweza kubadilisha kanisa lako kuwa “nyumba salama” - “Mji wa kukimbilia” Angalia (Hesabu 35) na pia mto wa uponyaji, tazama (Ezekieli 37: 1-12) utiririkao kuingia katika jamii.
Kuonyesha huruma na faraja ni Sanaa, hapa kuna baadhi ya mapendekezo :
Kuwa sahihi- sikiliza Zaidi ya vile unavyoweza kuongea,kuwa na uhakika na mwonekano wako (lugha ya mwili) iwe na hamasa ya kuonyesha upole na huruma.
Onyesha huruma nje ya mwonekano wako binafsi: Baadhi ya watu huonyesha huruma kimya kimya, wakilia na mtu mwenye matatizo, Wengine hawalii lakini huonesha huruma, kwa kuandaa kitu ambacho ni faraja kwa wafiwa.


Kuwepo mara nyingi ni muhimu Zaidi kuliko kuzungumza au kufanya
Ruhusu watu wahuzunike kwa namna zao wenyewe.
Zitambue vizuri hatua za machakato wa huzuni unao wapata watu.
Kuwa makini katika kusema, “najua jinsi unavyojisikia”uwezekano mkubwa ni kwamba huwezi.
Kuna mahali kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu


Usiseme nitakuombea, labda kama umekusudia kufanya hivyo kwa dhati, Kwa kadri inavyowezekana omba naye, mtembelee ukiwa huna haraka na shiriki pamoja naye ahadi za kwenye biblia zenye kutia moyo kwa watu wanao pitia mateso.
Andaa vikundi vya msaada (kama vipo) kwenye kanisa au katika jamii yako
.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA