![]() |
| WANKOTA KAPUNDA |
Na Magreth Yohana,Shua Media
“Mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponya nayo.Zaburi 34:22
“Mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponya nayo.Zaburi 34:22
Kama wanadamu tuliumbwa na kuweka katika dunia hii lazima
tupitie changamoto mbalimbli kiasi ambacho unaweza kukata tamaa na kuisi Mungu
kakuacha na labda ukawaza Mungu hayupo
kutokana na kuwa labda huna hela,huna kazi,haujui hata maisha ya kesho
yatakuwaje na huenda wakati huu umeshafukukuzwa sehemu uliyopanga kutokana na
kodi ama una umwa ugomjwa ambao unakosa tumaini la maisha
Wankota Kapunda ni binti mwenye umri wa miaka 24
ambaye amepooza miaka 4 iliyopita baada ya kupata ajali ya kugongwa na moja ya
gari wa mwanafunzi mwenzake ambayo walikuja
nayo ndugu zake na kumsababishia mifupa ya shingo kusagika na kuleta matatizo
kwenye uti wa mgongo aliyosabisha tatizo hilo siku ya mahafali yao ya kumaliza kidato cha
sita shule ya sekondari wasichana korogwe huko mkoani Tanga.
Baada ya Wankota kupata tatizo hilo alikaa
nyumbani kwa muda mrefu akiwa anangalia movie alitamani kuwa mwandishi wa
muswada wa filamu na alifanikiwa jambo hilo la kuandika muswada kwa kupitia
ulimi kutokana na upoozaji wa mwili mzima isipokuwa kichwa na hatimaye
kufanikiwa kuingia katika mashindano ya kitaifa ya kuandika muswada kwa haraka
na hatimaye kwa kupitia ulimi alifanikiwa kuwa mshindi kwa uandika haraka muswada wa huo yaliyofanyikia huko Zanzibari
yakishirikisha nchi za nchi za Afrika Mashariki.
Baada ya hapo Wankota hukukata tamaa tena aliendelea kuwaza
vitu vikubwa vitavyoweza kuisaidia jamii na watu wenye hali kama yake ambao
wametengwa na familia zao kutokana na kuwa tatizo kama la kwake, ambalo linaitaji
msaada mkubwa na jamii inapaswa
kuelimishwa jinsi ya kuwajali na kuwahudumia
vema watu wenye tatizo kama la
Wankota kwa kupitia uigizaji wa movie ambao
ataufanya alisema wankota.
Hayo nimewambieni mpate kuwa na Amani ndani
yangu,Ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo na mimi nimeushinda ulimwengu.>>>Yohana
16:33.
Tumaini lipo jipe moyo ukijua Yesu amekushindia yote ya
dunia yanapita na hayana budi kutokea alishinda ulimwengu hatakuacha usilie
tena, usihuzunike kwa kuwa amesema yeye ameshinda ulimwengu, atakupa njia ya
kukabiliana nayo yote endapo tu utaamua kumtumaini na kuomba katika kweli.
Zaburi 24:1.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***





0 comments:
Post a Comment