Saturday, September 24, 2016

Kikundi cha waimbaji wa Born to Praise toka jijini Da Es Salaam hapo jioni ya kuamkia leo waliwasili Lolwe Shirati na kufikia kwenye mji wa wazazi wa Bambino Phillip Nyambita (Katibu wa Born To Praise) na Naftal Phillip Nyambita (Mwenyekiti wa Born To Praise). Waimbaji hawa waliambatana na timu ya Infinite Production na timu ya injilileo Blog ambao walikaribishwa chakula cha jioni katika mji huo na wasaa wa kutambulishwa ukafika, katibu wa Born To Praise Mr Bambino Phillip Nyambita aliwakaribisha wageni hawa akiwa yeye ndiye mwenyeji na alitoa neno la shukrani kwa kwaya ya Ochune ambao walikuja kuwasalimia na kujumuika nao katika jioni hiyo.
Kulia ni Mr Bambino alipokuwa akisema machache kwa utambulisho wa Born To Praise kwa wanyeji na pia kwaya Ochuna kwa wageni.
Kutoka kushoto ni Katibu wa kikundi cha Born to Praise Bambino Phillip Nyambita, Bibi Phillip Nyambita na Mzee Phillip Nyambita walipokuwa katika utambulisho.
Huyu ni Mr Bambino alipokuwa akisema machache kwa utambulisho wa Born To Praise kwa wanyeji na pia kwaya Ochuna kwa wageni.

Familia ya Bwana na Bibi Phillip Nyambita walipokuwa wakipita mbele kwa utambulisho.
Kutoka kushoto ni Katibu wa kikundi cha Born to Praise Bambino Phillip Nyambita, Bibi Phillip Nyambita na Mzee Phillip Nyambita walipokuwa katika utambulisho.
Waimbaji wa Kikundi cha Born to Praise walipokuwa wakitoa huduma ya uimbaji hapo jana usiku katika mji wa Bwana na Bibi Phillip Nyambita.
Waimbaji wa Kikundi cha Born to Praise walipokuwa wakitoa huduma ya uimbaji hapo jana usiku katika mji wa Bwana na Bibi Phillip Nyambita.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA