Thursday, December 22, 2016



* Kuepuka uzinifu inawezekana kama utadhiria kufanya hivyo maana ni jambo ambalo liko ndani ya uwezo wako.
Hizi ni baadhi ya njia za kukusaidia
* Jaza moyoni mwako neno la Mungu siku zote, hii itaziba mianya yote ya mawazo/tamaa mbaya akilini mwako! (Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu Na mwangaza wa njia zetu)
(Hii inabeba zifuatazo)
¶. Usitumie muda mwingi kuwa Na marafiki wa jinsia tofauti Na yako wakati mke/Mme wako hajui kama uko huko, (Mme/mke wako ndio best Friend wako spend muda wako Na yeye)
¶. Usikae mahali pasipokuwa pa wazi (open place) Na MTU wa jinsia tofauti Na yako ni hatari kwako
¶. Usiongee mbele ya marafiki zako juu ya madhaifu ya mwenzi wako (mf. Haniridhishi, hanipi furaha, hanijali n.k) marafiki hao wanaweza kuchukua nafasi hiyo kukuonesha upendo fake Na kukupa kile ulichokua unahisi kuwa unakikosa kwa mwenzi wako, unafungua milango Na madirisha kwajili ya ibilisi! Ni hatari
¶. Ishi maisha ambayo yanakutambulisha wewe kama ni mke/Mme wa mtu, (kuna wengine wameoa lakini mpaka leo status zao zimeandikwa "Single" wengine wakulizwa umeoa/umeolewa wanasena "Hapana" hivi hua mnamanisha nini? Unafikiri kuna mwingine ajae? Jivunie kuwa nae huyo ndie mwenyewe wala hakuna mwingine.

¶. Usitembelee website za ngono au kuangalia mapicha ya uchi uchi (phonograph) hizo zitakujengea mawazo mabaya Na mwisho wa siku unaamua kwenda kufanya kwa vitendo (practical) kile ulichokiangalia, ni hatari kwako.
¶. Usiwe msiri kwa mwenzi wako kuwa mkweli Na muwazi ninyi ni mwili mmoja so kama unaona hauridhiki Na Huduma zake kaa nae chini mweleze vile ambavyo unajisikia kuliko kuamua kwenda kutafuta kuridhishwa nje unapotea (mtengeneze jinsi utakavyo yeye awe)
¶. Usipokee vizawadi zawadi au offer Mbali mbali kutoka kwa jinsia yako tofauti IPO Siku watakuomba uvirudishe vitu hivyo (Na hawatataka vitu) watahitaji uvilipe kwa ngono, umejichimbia kaburi mwenyewe, usipende vya bwelele Hakuna cha bure duniani Mungu pekee ndio hutoa kila kitu bure!
¶. Usifikirie kwamba huenda kuna mke/Mme nzuri zaidi ya huyo ulienae, Amini Mme wako ndio handsome kuliko wote unawaona duniani Na Mme amini kuwa mke wako ndio Miss world hakuna wa kufanana nae tena dhamiria kwamba yeye pekee anakutosha.
¶. Hakikisha mahitaji yake yote yanapatikana kwako, kisiwepo kitu atakacho kikosa kwako, mahitaji yote mtumizie ili asiwe Na sababu ya kwenda kutangatanga huko nje!
¶. Kumbuka chochote alichonacho mwanaume/mwanamke yeyote ktk mwili wake basi Mme/Mke wako anacho pia Na hakuna utofauti kabisa tofauti ni sura zao tu basi lkn vilivyomo ndani ni vile vile , so usitoke nje ukafikiria utapata kitu special unajidanganya, tulia nyumbani
¶. Wakati mwingine unajisikia kummiss (kumkosa) mkeo/mmeo hali hiyo inajitokeza wakati Mme/mke wako hayupo, hiyo isiwesababu ya kukufanya utoke nje jitahidi kujikeep busy Na hali hiyo itapotea 

Ukiwa Na fikra za kingono Na MTU asie mmeo/mkeo jitahidi kuua hizo fikra kabla hazijakuua
¶. Ukiwa Na safari ya mbali Na mwenzi wako kabla hujasafiri tenga muda wa kuwa Na mwenzi wako kwa kadri uwezavyo Na wakati huo dhamiria moyoni Na akilini kwamba hutafanya hicho kitu huko utakakokua mpaka utavyorudi nyumbani (tengeneza memory hiyo itakusaidia ukiwa mbali Na mwenzako)
¶. Wanaume epuka kutazama vifua Na makalio ya wanawake wasio wake zenu, mtamani mkeo tu (Na kama mkeo humtamani basi hana tofauti Na Dada yako, ) unaouwezo wa kumfanya mkeo akuvutie Siku zote, mtengeneze jinsi utakavyo yeye awe, kama mwembamba ndio anakuvutia Na mkeo ni bonge mfanyishe mazoezi atakua basmati Na atakuvutia pia
¶. Usiwe Na marafiki wasio Na hofu ya Mungu, wanaweza kukushawishi vibaya, Usiwe marafiki wasio olewa bado (mawazo mabaya huharibu tabia njema)
#KUMBUKA
Kitendo cha akichukui masaa Mengi kufanyika lakini hasara yake ni ya milele, starehe ya lisaa limoja itakuangamiza milele, #Uzinifu_ni_Dhambi. Mshahara wa dhambi ni Mauti rafiki!
#Uaminifu_unalipa
Bwana abariki ndoa zilizopo Na zile zijazo kwa utukufu wa jina lake! Amen
Na Catheline Masiko 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA