Wednesday, January 25, 2017


Wazazi wote nawaomba msikose somo hili ni la muhimu sana?
SOMO HILI LIMEGAWANYIKA SEHEMU MBILI
Mambo unayopaswa kuwafanyia watoto wako
Mambo ambayo hupaswi kuwafanyia watoto wako
MAMBO UNAYOPASWA KUWAFANYIA WATOTO WAKO;
i. KULEA WATOTO KATIKA NJIA SAHIHI
MITHALI 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee
ii. KUWAFUNDISHA WATOTO
TORATI 6:7-9 Nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.soma maelezo ya ziada kutoka
KITABU CHA KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA KWANZA SURA 13,UK,100 (JIFUNZE KWA BIDII NA KWA UTARATIBU)
Wazazi kama mkitaka kuwafundisha watoto kumtumikia Mungu ifanyeni BIBLIA kitabu chenu cha mafundisho,inafunua hila za shetani ,ni kitu kikubwa chenye kuliinua Taifa cha kugombeza na chenye kutoa makosa ya tabia ya moyoni kitu cha kuvumbulia ambacho hutuwezesha kupambanua baina ya kweli na uongo ,LOLOTE lifundishwalo nyumbani au shuleni ,BIBLIA ikipewa nafasi hii Mungu hutukuzwa ,naye atawafanyia kazi katika kuwaongoza watoto wenu,kuna shimo la mali ya kweli na uzuri katika hiki kitabu kitakatifu na wazazi yawapasa kujilaumu wenyewe kama wasipokifanya kuwa cha kuwapendeza kabisa watoto wao.........kuwafundisha ukweli wa biblia ni kazi kuu na ya maana ambayo kila MZAZI ANAPASWA KUFANYA,kwa moyo mzuri,wa furaha uyaweke maneno ya kweli kama yalivyosemwa na Mungu mbele ya watoto.kama BABA NA MAMA MWAWEZA KUWA MFANO wa mafundisho kwa watoto katika maisha ya kila siku kwa kutumia ,uvumilivu,huruma,na upendo kwa kuwavuta kwako.Msiwaache kufanya wapendavyo.
iii. WAJIBU WA WATOTO KWA WAZAZI WAO
WAEFESO 6;4 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana
iv. MRUDI MWANAO KUNGALI BADO KUNATUMAINI
Kutoa adhabu kwa mtoto sio dhambi wazazi naomba muelewe hilo
MITHALI 22:15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali
MITHALI 13;24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema
MITHALI 19:18 Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake
WAZAZI HAWAPASWI KUWAFANYIA WATOTO WAO MAMBO YAFUATAYO
v. WAZAZI HAWAPASWI KUWACHOKOZA WATOTO WAO
WAEFESO 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; Bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana
WAKOLOSI 3;21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
vi. TABIA MBAYA WALIZONAZO WAZAZI ZITAPATILIZWA KATIKA VIZAZI VYAO,(jambo hili linahuzunisha mno angalia jinsi lilivyo)
KUTOKA20:5-6 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; NAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.ANGALI MALEZO YA ZIADA
KITABU CHA KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA KWANZA ,SURA YA 17,UK 127(MATOKEO YANAYOLETWA NA UCHAFU WA TABIA)
UASHERATI UMEFANYA MENGI ZAIDI YA UOVU WOWOTE mwingine kuziharibu tabia za wanadamu ,unatendeka kwa kadiri kubwa ya kutisha nao huleta magonjwa karibu ya kila aina
KWA KAWAIDA WAZAZI hawadhani kuwa watoto hawafahamu lolote juu ya uovu wao huu ,mara nyingi wazazi ndio wenye makosa hasa ,WAMETUMIA VIBAYA HAKI YA NDOA YAO na kwa uzoefu wa kujifurahisha kwa anasa wameziimarisha tamaa zao mbaya za mwili yaani ashiki.Na kadiri hizi zilivyoimarika ,Ndivyo tabia ya moyoni na uwelekevu vilivyodhoofisha .Hali ya kiroho imeshindwa na tabia ya kinyama ,WAKIWA WANAYO CHAPA YA TABIA YA WAZAZI WENYEWE,watoto wanazaliwa kwa wazazi hawa karibu siku zote WATARITHI MAZOEA HAYA YA KUCHUKIZA YA UOVU WA SIRI ,Dhambi za wazazi hawa ZITAPATILIZWA KWA WATOTO WAO kwa sababu wazazi hawa wamewapa chapa ya tamaa mbaya walizonazo wao wenyewe
Wale wanaoimarika kabisa katika dhambi hii inayoharibu mwili na roho hawawezi kupata raha ila kwa shida mpaka mzigo wao wa dhambi hii ya siri umefunuliwa kwa wale wanaoshirikiana nao.
KITABU CHA KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA KWANZA ,SURA YA 23,UK158(MAMA NA MTOTO WAKE)
Ikiwa kabla ya kuzaliwa kwa mtoto wake ,mama mwenyewe ni mfisadi kama ni mchoyo,mwenyewe harara na mkali ,tabia hizi zitaonekana kwa mtoto.hivyo watoto wengi wamerithi mielekeo mibaya wasiyoweza kuishinda ila kwa shida sana
Lakini ikiwa mama hushika bila kusitasita kanuni ,kama akiwa mwenye kiasi na mwenye kujizuia ,kama ni mwenye utu wema ,mpole , na mkarimu ,aweza kumrithisha mtoto wake tabia hizo za thamani kuu
Watoto wachanga ni kioo kwa mama ambamo huweza huweza kuona sura ya mazoea na mwenendo wake mwenyewe.BASI ANGEJIHADHARI kama nini na maneno yake pamoja na mwenendo wake mbele ya hawa watoto wadogo ,tabia zozote atakazo kuona wanazo hana budi kuwa nazo yeye mwenyewe.
vii. KUWALEA WATOTO KAMA MAYAI NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU
SOMA KITABU CHA KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA KWANZA SURA YA 37 ,UK238(HESHIMA YA KAZI)
Ni dhambi kuwaacha watoto kukua kivivu,hebu wavizoeze viungo vyao na misuli ,hata kama inawachosha .ikiwa hawatumikishwi kupita kiasi ,uchovu wawezaje kuwadhuru kuliko wewe?kuna tofauti kabisa baina ya uchuvu na ulegevu.watoto wanahitaji mageuzi ya kazi mara kwa mara na vipindi vya mapumziko zaidi kuliko watu wazima wanavyohitaji,lakini iwapo bado ni wachanga ,waweza kuanza kujifunza kufanya kazi na watakuwa na furaha mawazoni mwao kwamba nao wanaweza kujifanya kuwa wenye manufaa .usingizi wao utakuwa mtamu baada ya kufanya kazi baada ya kutia afya na watakuwa wameburudishwa kwa kazi inayofuatia
viii. NJIA YA TEKENOLOJIA INAWAATHILI WATOTO WENGI MNO
Kuwanunulia watoto CD ambazo hazina maadili au kuwaruhusu kuangali picha mbaya mfano picha za mauji,uchawi.na mengine.watoto wanapoangalia hivyo vitu


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: , ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA