Wednesday, February 08, 2017


Nakukumbusha!
Kama mke wako matarajiwa hana hizi SIFA japo kwa mbali "FIKIRIA MARA MBILI"
~Anaependa mambo ya kiroho
~Upendo wa kweli, (si mpenda vitu) ukija na kitu unaitwa Majina special honey, Darling sweetie n.k ukija mikono mitupu anakungalia kama hakuoni wakati anakuona
~Mtiifu (wanaume hawapendi kurudia rudia Mara mbili mbili kwa jambo lile lile)
~Mwaminifu katika yote (kwa vitu vidogo na vikubwa)
~Anaejituma, (asie mke mvivu)
~Mnyenyekevu (Anaejishusha, sio Mme anaongea naye anaongea mnashindana)
Ajue wapi pa kuongea na wapi anyamaze

~Mwenye heshima kwa Mme (ajue mme ndo kichwa cha Nyumba na haitabadilika) aheshimu na watu wengine pia
~Asiye na tamaa au kupenda pesa kuliko utu, ama kupenda mafanikio ya shortcut au kupenda vitu vikubwa kuliko uwezo wa mme
~Mkarimu
~mvumilivu ktk hali zote (Anaejua kuna kupata na kukosa)
~Mwenye kumshauri Mme au kumtia MOYO
~Asie na marafiki wabaya (mashostito) hasa wenye mitazamo hasi
~Anaejali/asie na ubaguzi wa ndugu (anawapenda wa kwao lakini ndugu wamme hawapendi)
~Mwenye shukrani
~ Msafi (wanaume hawapendi uchafu)
~Mwenye uwezo wa kutatua matatizo ya familia yake yeye na Mme wake si lazima apeleke kwa ndugu zake au wazazi (mwanamke mwenye hekima aijenga Nyumba yake mwenyewe Bali mpumbavu ataibomoa)
~Mwenye kutunza siri za familia yake!
~Mbunifu/ ajue kupika sababu Mme wake anatamani kula chakula chake si cha house girl (kama hajui kupika anaweza kujifunza na akajua si shida sana)
~Anaejua majukum yake kama mke (Mme hajamuoa house girl kakuoa Wewe AJITAMBUE)
~Mwenye uzuri wa asili (asijipambe ajitunze)
~Mwenye kujiheshim kuanzia muonekano wa nje wa mavazi yake na kuongea pia (kuna wanawake wanaongea bila kituo una neno 1 ana maneno 30)
Ajue kuvaa vizuri mke akivaa vibaya Mme wake itakuwaje? Sababu mke ndio kioo cha mwanaume kumwangalia amevaaje!
Hizo ni chache kati ya nyingi, na usitegemee atakuwa nazo zote (akiwa nazo zote atakuwa si mwanadam) lakin angalia zile za mhimu na ufikirie Mara mbili
Usiache kumuombea kila siku tena kwa kumtaja kwa jina lake!
Bwana awafanikishe katika mipango Yenu kwa kadri atakavyo yeye wala si vile matakavyo ninyi! Neema yake isiwapungukie #AMEN
Na Catherine Masiko

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA