Sunday, June 19, 2022

 Soma Mwanzo 46. Kuondoka kwa Yakobo Kanaani kuna umuhimu gani?

 

Yakobo anapoondoka kwake Kanaani, amejawa tumaini. Uhakikisho kwamba hataona njaa tena, na habari njema kwamba Yusufu yu hai, ni lazima vilimpa msukumo kwamba anapaswa kondoka katika Nchi ya Ahadi.

Kuondoka kwa Yakobo kunatoa mwangwi wa uzoefu wa Ibrahimu, ingawa kwa habari ya Ibrahimu alikuwa anaelekea katika Nchi ya Ahadi. Yakobo anasikia ahadi ile ile ya Ibrahimu ambayo Ibrahimu aliisikia toka kwa Mungu, yaani kwamba atamfanya kuwa “taifa kubwa” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 12:2). Wito wa Mungu hapa pia ni ukumbusho wa agano la Mungu na Ibrahimu; katika matukio yote Mungu anatumia neno lile lile linalotoa uthibitisho tena “ ‘usiogope’ ” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 15:1), linalobeba ahadi ya maisha yajayo yenye utukufu.

Kuorodheshwa kwa upana kwa majina ya watoto wa Israeli walioenda Misri, pamoja na binti zake (Mwa. 46:7), kunakumbusha ahadi ya Mungu ya uzao mwingi kwa Ibrahimu hata wakati akiwa bado hana mtoto. Namba “sabini” (pamoja na Yakobo, Yusufu, na wanawe wawili) inaelezea wazo la utimilifu/ukamilifu. Ni “Israeli yote” inayokwenda Misri. Ni muhimu pia kwamba namba 70 inafanana na namba ya mataifa (Mwanzo 10), kuashiria kwamba hatima ya mataifa yote ina hatarishwa katika safari ya Yakobo.

Ukweli huu utakuwa dhahiri zaidi tu miaka mingi baadaye, baada ya msalaba na ufunuo kamili zaidi wa mpango wa wokovu, ambao, bila shaka, ulikuwa kwa ajili ya wanadamu wote, po pote, na si tu kwa watoto wa Ibrahimu.

Kwa maneno mengine, hata kama visa vinavyohusu familia hii vinavutia, uzao wa Ibrahimu, na masomo yo yote ya kiroho tunayoweza kujifunza kutokana nayo—simulizi hizi ziko katika neno la Mungu kwa sababu ni sehemu ya historia ya wokovu; ni sehemu ya mpango wa Mungu wa kuleta ukombozi kwa watu wengi iwezekanavyo katika sayari iliyoanguka.

“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, ‘Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka’ ” (Rum. 10:12, 13). Paulo anasema nini hapa kinachoonesha kuwa injili ni kwa ajili ya ulimwengu wote? Muhimu zaidi, maneno haya yanatuambia nini kuhusiana na kile ambacho sisi kama kanisa tunapaswa kufanya ili kusaidia kuitangaza injili?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, May 06, 2022




Siku ya kesho ambayo ni sabato ya Mungu pamoja na mambo mengine itakuwa maalum kwa ajili ya kuchangia vyombo vya habari vya kanisa la Waadventista wasabato Tanzania.
Sadaka yako itasaidia katika upanuzi wa masafa ya redio ya Morning Star na injili itaweza kufika mbali na Yesu atarudi upesi. Karibu kuungana nasi kuchangia.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, July 19, 2020



Mtoto Yusuph toka jijini Dodoma amefika Dar es Salaam na jana July 18, 2020 amehudumu kwa njia ya wimbo katika kanisa la Waadventista wa Sabato Temeke. Mungu aendelee kumtunza na karama hii iende mbali.


MTAZAME HAPA AKIIMBA ****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, July 17, 2020

Sisi tumeacha vyote tumeamua kukufuata wewe Bwana, tutapata nini kwako??
Ni maneno yaliyo kwenye video ya wimbo mpya ya waimbaji wa Ellen Singers toka Golani Dar Es Salaam.Kuutazama wimbo huu tazama hapa



. Waimbaji wa Ellen singers waliwahi kuwa na mipango katika utume wao wa injili ****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, July 16, 2020

Makambi mtaa wa Kahama Kati mkoani Shinyanga yameanza tangu tarehe 12 na yataisha tarehe 19 mwaka huu wa 2020. Wachungaji mbali mbali kama; Mchungaji Lucas Rugemalila, Mchungaji Nuhu Suleimani, Mchungaji Elikana Kuzenza na Mchungaji mwenyeji wa mtaa Mchungaji Reward Mmbaga. Fuatilia matukio kwa njia ya picha kwenye blog yetu. Picha zote na Presenter yohana - Matendo ya kanisa
Karibu makambi ya kahama kati 2020
Karibu makambi ya kahama kati 2020



Karibu makambi ya kahama kati 2020








****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, July 14, 2020

Mtoto Yusuph ni mwenyeji wa Dodoma na mtoto wa pili katika familia yao.
Mtoto huyu alipata kufahamika zaidi pale alipoonekana akiimba wimbo wa "Tusifanane na Mafarisayo"
"Sazingine siendi kanisani kwa kukosa nguo na wakati mwingine nguo huwa ni chafu" Mtoto Yusuph alisema.



KIJANA YUSUPH ALIFAHAMIKA SANA KWA KUONEKANA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII AKIIMBA WIMBO HUU KWENYE VIDEO HII HAPA MFAHAMU ZAIDI MTOTO YUSUPH


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Monday, June 12, 2017








Tuesday, March 28, 2017

Isaya 54:10 "Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali WEMA wangu HAUTAONDOKA kwako, wala AGANO langu la AMANI halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye".
Rafiki; bila kujali hali ya maisha unayoipitia, changamoto zisizoisha, huenda unaomba Maombi na Mungu anaonekana amekaa Kimya - Neno linasema WEMA wa Mungu HAUTAONDOKA KWAKO.  
Kumbuka maisha ya nyuma uliyopitia, ni hakika kuna wakati mgumu ulikuwa mbele yako ukiwa umekosa matumaini, lakini leo hii imebaki kuwa historia. Inua macho yako juu, tazama ahadi za Mungu wako - Naye atalitimiza Neno lake kwa wakati usioudhani. Songa mbele kwa IMANI isiyoyumba, naye ATATENDA.
NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE
Na: 
Ev. Eliezer Mwangosi
+255766992265

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, March 14, 2017


SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA