Monday, November 30, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, November 29, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani [mkamilifu]? naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii. Isaya 42:19,20 [KJV].

Ni upofu gani huu? Ni upofu ambao hautayaruhusu macho yetu kutazama sana maovu. Hautayaruhusu macho yetu kutulia juu ya maovu. Hautayashika mambo yale yanayoonekana na kuupoteza umilele katika kumbukumbu zake.... Tunataka kuona ipasavyo, tunataka kuona kama vile aonavyo Mungu; maana Shetani anajaribu daima kuyageuza mambo yale ambayo macho yetu yanayaangalia sana ili tupate kuyaona kwa njia yake aliyoichagua....

Mtumishi wa Mungu aliye hai anaona akiwa na kusudi fulani. Macho hutakaswa na masikio nayo hutakaswa, na wale watakaofumba macho na masikio yao wasiyaangalie maovu watabadilika. Lakini endapo watawasikiliza wale wanaozungumza nao na wanaojaribu kuyaongoza mawazo yao mbali na Mungu na mbali na mambo yao yale ya milele, basi, hapo ndipo fahamu zao zote zitapotolewa kutokana na kile macho yao yanachokiangalia sana. Yesu asema, "Basi... jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza." Mathayo 6:22,23.

Inaleta tofauti kubwa juu ya kile tunachoilisha mioyo yetu na roho zetu. Tunaweza kuiacha mioyo yetu kutafakari sana hadithi zile za mahaba na ndoto zisizowezekana, je! hayo yatatufanyia nini sisi? Yatatuangamiza, mwili na roho.... Twataka kuwa na nguvu ile itakayotuwezesha kuyafumba macho yetu kwa mandhari [picha] zile zisizokuwa nzuri; zisizotuadilisha tabia zetu, zile ambazo hazitatutakasa na kutufanya kuwa waungwana; na kuziba masikio yetu kwa kila kitu kilichokatazwa katika Neno la Mungu. Anatukataza kuwaza maovu, kusema maovu, na hata kutafakari maovu....

Ndani ya Yesu mimi naona kila kitu kilicho chema, kila kitu kilicho kitakatifu, kila kitu kinachotia moyo na kilicho safi. Basi, kwa nini mimi nipende kuyafumbua macho yangu sana ili kuangalia kila kitu kinachochukiza? Kwa kutazama tunabadilishwa. Na tumtazame Yesu na kuutafakari uzuri wa tabia yake, na kwa kutazama tutabadilishwa tupate kufanana na sura yake.

BWANA AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA BARAKA TELE


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Saturday, November 28, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Wakati wa huduma ya ibada ilipokuwa inaanza, wapendwa hawa waliweza kukiri kumfuata Bwana Yesu kwa kiapo cha ubatizo na mara baada ibada ya leo mchana ubatizo huu utafanyika.
Picha na Godson Mhezi

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Tafakari: 2Wakorintho 10:3-5
 "Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; maana Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina UWEZO KATIKA MUNGU hata kuangusha Ngome; tukiangusha Mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu;  na tukiteka nyara kila FIKIRA ipate KUMTII Kristo". 

Nakumbuka usemi wa marehemu Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere, wakati Raisi wa Uganda Idd Amini alipoivamia Tanzania, Baba wa Taifa alisema "Nia tunayo, Sababu tunayo na Uwezo wa kumpiga tunao". Ndipo akatoa Amri ya Kumpiga na Kuivunjilia mbali ngome yake katika nchi yake.

Katika ulimwengu wetu huu uliotekwa na Adui shetani, ni jambo la kawaida kusikia Watu wanajiita ni Wakristo, wengine wanajiita wacha Mungu, wengine wameokoka n.k. Wanauwezo mkubwa hata wa kuimba nyimbo za dini kwa hisia kubwa, lakini jambo la kushangaza, asilimia kubwa unawakuta bado ni watumwa wa yule Adui. 

Mbali na kuonekana watu wema au wacha Mungu machoni pa watu, ndani ya Mawazo yao au Fikira zao, kumejaa Visasi, Uadui, Kutosamehe, Husuda, Wivu. Wakati mawazo, maneno na matendo ya Ngono na Mapenzi yakiendelea kukamata akili za Vijana kwa Wazee, wakipigwa upofu wasione kuwa ni dhambi; Mungu anazidi kutoa wito wa Kushinda vita. 

Wapendwa Ngome kuu za Shetani ziko katika MAWAZO au FIKIRA, huko ndiko zinatakiwa zivunjiliwe mbali, hatimaye mawazo yetu yaunganishwe na Kristo. Hayo yanawezekana tu kwa watu ambao wameruhusu utawala wa Ufalme wa Mungu kuwa ndani yao, kwa njia ya Roho mtakatifu. 

Ni wakati wa kila mmoja kujipima, kuwa je; ni kweli amezivaa Silaha zenye Uwezo wa Mungu? Mawazo na Fikira Je zinapatana na Mungu au zimejaa Uchafu wa yule Adui shetani? Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya kutuokoa kutoka katika mateka ya dhambi, na huu ndio uhuru wa Kweli.

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA MAFANIKIO KATIKA MWILI NA ROHO. 

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, November 27, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Yamesalia masaa machache kuifikia Sabato ya tarehe 28, ambayo ni sabato maalum ya uimbaji katika shule ya msingi Kongowe, shule inayomolikiwa na kanisa la Waadventista Wasabato iliyopo Kongowe Pwani.

Pamoja na waimbaji wengi watakaoshiriki katika siku hii, pia watakuwepo Glory Land Singers kutoka katika kanisa la Waadventista Wasabato Tegeta jijini Dar es Salaam, Faraja Singers ya Kongowe kati, Kwaya ya Nuru ya Kongowe na Kwaya ya Shule ya Kongowe.

Kama unahitaji muziki wa Kikristo, KARIBU KAPS JUMAMOSI HII.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Tafakari: Marko 11:25 "Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu".

Kama kuna dhambi itakayowapeleka wengi motoni, ni hii ya kutosamehe. Ingelikuwa mtu anapewa kuona yaliyo ndani ya mioyo ya watu; tungeshuhudia majeraha makubwa yasiyopona, yaliyotokana na kuumizwa na ndugu au jamaa na wakati mwingine wapenzi wao. Japokuwa hatuwezi kuona, maneno ya manung'uniko na malalamiko yanafunua mizigo ilioko ndani japo kwa sehemu ndogo.

Wengi utasikia wanasema "nimemsamehe ila sitasahau" huyo bado anamaumivu hajasamehe. Wengi wanaenda majumba ya Ibada, wanaimba, wanahubiri, wanatoa zaka na sadaka, huku wakiwa bado wana mafukuto ya chuki kwa waliowakosea. Utakuta mtu anajisifia akisema "mimi hata simsalimii" au "nikimuona nakereka", ndivyo wengi walivyo hata kama hawasemi. Jiulize ukimuona yule mbaya wako unajisikiaje? Kila mmoja analo jibu.

Haijalishi umeumizwa kiasi gani; iwe ni kazini, iwe kwenye ndoa au mahusiano, au katika mazingira yoyote; unapaswa kusamehe kabisa, na kuachilia roho za kulipa kisasi, manung'uniko, malalamiko, chuki, hasira na harara. Hayo yote yakidumu moyoni yanafunga kabisa milango ya mbinguni.

Yesu alirudia kufundisha jambo hili akiwa anawafundisha wanafunzi wake kuomba akisema - Mathayo 6:12 "utusamehe deni (makosa) yetu, kama sisi nasi tuwasemehevyo wadeni (waliotukosea) wetu". Kwa maneno hayo, tunajifunga kitanzi au kuwa huru, kwa kusamehe au kutosamehe.

Wapendwa katika hali ya ubinadamu jambo hili la msamaha ni gumu, hivyo linahitaji kutoa maisha yetu kwa Yesu Kristo ili atupatie uwezo wa kutenda yale tusiyoweza, atupatie tabia ya Upendo wa kuwapenda wabaya na kuwaombea. Msamaha ni mojawapo ya vipimo kama kweli tunaongozwa na Roho mtakatifu au bado tuko chini ya kongwa la utumwa.

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE NURU YA MAFANIKIO NA BARAKA TELE.

By: Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, November 26, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, November 25, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, November 24, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Monday, November 23, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Katika ibada ya Sabato ya tarehe 21 kanisa la Ilala SDA la jijini Dar es Salaam limeweka wakfu kwa Mungu  vyombo vipya vya mawasiliano, ikiwemo Mixer kubwa yenye njia 24, Spika kubwa 2, Spika ndogo 2, Amplifaya 1, Snake Cable 1.

Awali akitoa taarifa ya kile kilichonunuliwa, mkuu wa mawasiliano kanisani hapo Bwana Elishama Marwa alisema wanashukuru kwa upatikanaji wa vifaa hivyo ila bado wanahitaji kubwa la vifaa vingine kama Vipaza sauti na stendi zake hivyo kutoa wito kwa watu wengine kujitokeza kusaidia kuondoa hitaji hilo.

Mchungaji wa kanisa, Mch. Shehemba katika huduma yake ya kuviweka wakfu vifaa hivyo alikazia kuhusiana na matumizi ya vifaa hivyo ya kwamba ni kwa ajili ya Mungu pekee hivyo kuwaomba waangalizi wa vifaa hivyo hasa idara ya mawasiliano kuwa makini sana na matumizi ya vifaa hivyo.

Timu ya injilileo, tunawapongeza kwa hatua hiyo na kuwaombea kwa Mungu vifaa hivyo vitumike kama ilivyokusudiwa kwa kusudi la injili.
Mixer ya zamani ikiwa katika matumizi ya sabato hiyo
Kijana Samwel akipiga kinanda katika Ibada
Viongozi wa Idara ya mawasiliano kanisani wakiondoa vitambaa kuwaonesha washiriki vifaa vilivyonunuliwa na hatimaye kukabidhiwa kwa Mungu
Vifaa vilivyonunuliwa katika awamu ya kwanza
Kiongozi wa Mawasiliano Elishama Marwa akitolea maelezo vifaa vilivyonunuliwa na nyuma yake ni Mchungaji wa kanisa Sadickiel Shehemba
Kiongozi wa Mawasiliano Elishama Marwa akitolea maelezo vifaa vilivyonunuliwa na pembeni yake ni Mchungaji wa kanisa Sadickiel Shehemba
Mchungaji wa Kanisa Sadikiel Shehemba
Mchungaji akianza Huduma maalum
Monitor Speaker
Maombi yakiendelea

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, November 22, 2015

Tafakari: Marko 11:25 "Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu".
Kama kuna dhambi itakayowapeleka wengi motoni,  ni hii ya kutosamehe. Ingelikuwa mtu anapewa kuona yaliyo ndani ya mioyo ya watu; tungeshuhudia majeraha makubwa yasiyopona, yaliyotokana na kuumizwa na ndugu au jamaa na wakati mwingine wapenzi wao. Japokuwa hatuwezi kuona, maneno ya manung'uniko na malalamiko yanafunua mizigo ilioko ndani japo kwa sehemu ndogo.

Wengi utasikia wanasema "nimemsamehe ila sitasahau" huyo bado anamaumivu hajasamehe. Wengi wanaenda majumba ya Ibada, wanaimba, wanahubiri, wanatoa zaka na sadaka, huku wakiwa bado wana mafukuto ya chuki kwa waliowakosea. Utakuta mtu anajisifia akisema "mimi  hata simsalimii" au "nikimuona nakereka", ndivyo wengi walivyo hata kama hawasemi. Jiulize ukimuona yule mbaya wako unajisikiaje? Kila mmoja analo jibu.

Haijalishi umeumizwa kiasi gani; iwe ni kazini, iwe kwenye ndoa au mahusiano, au katika mazingira yoyote; unapaswa kusamehe kabisa, na kuachilia roho za kulipa kisasi, manung'uniko, malalamiko, chuki, hasira na harara. Hayo yote yakidumu moyoni yanafunga kabisa milango ya mbinguni.

Yesu alirudia kufundisha jambo hili akiwa anawafundisha wanafunzi wake kuomba akisema - Mathayo 6:12 "utusamehe deni (makosa) yetu, kama sisi nasi tuwasemehevyo wadeni (waliotukosea) wetu". Kwa maneno hayo, tunajifunga kitanzi au kuwa huru, kwa kusamehe au kutosamehe.

Wapendwa katika hali ya ubinadamu jambo hili la msamaha ni gumu, hivyo linahitaji kutoa maisha yetu kwa Yesu Kristo ili atupatie uwezo wa kutenda yale tusiyoweza, atupatie tabia ya Upendo wa kuwapenda wabaya na kuwaombea. Msamaha ni mojawapo ya vipimo kama kweli tunaongozwa na Roho mtakatifu au bado tuko chini ya kongwa la utumwa.

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE NURU YA MAFANIKIO NA BARAKA TELE.

By: Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299. 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Saturday, November 21, 2015

Tafakari: Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo mtazidishiwa".

👉Kila kunapokucha maisha ya mwanadamu yanazidi kukutana na changamoto za kukatisha tamaa. Kuanzia maisha ya mtu binafsi, familia, taifa hadi mataifa n.k. Kila siku zinaibuka changamoto mpya zinazoumiza vichwa.

👉Bila kujali; uzuri wa maumbile, hali ya kifedha, elimu waliyonayo, mali wanazomiliki, demokrasia walizonazo, uwe katika ndoa au laa, uwe na mchumba au katika mahusiano yoyote, mwanadamu awe na hali yoyote ile, ni hakika anayo changamoto, na kama kwa sasa hana; atakuwa amaisha ipitia au ziko mbele zinakuja.

👉Sikiliza; Watu wanatafuta AMANI, lakini Kila leo amani inazidi kupotea, wengi wanatembea wakiwa na maumivu moyoni, kila mmoja akiwa amejeruhiwa na jambo fulani. Hata siku hii leo wengi wana mizigo mizito, hawajui mwisho wake. Vijana wana changamoto, watu wazima ndio usiseme, viongozi wa mataifa makubwa kwa madogo hawalali.

👉Hitaji letu kuu ili kupita salama katika dhoruba hizi za ulimwengu ni kumrudia Mungu, kuutafuta ufalme wake kwanza, adha zote tunazozipata ni mishale ya adui shetani, inayotupata kwa HILA. Amani ya kweli na ya kudumu bila Mungu, ni kujilisha upepo. Wanaodai wana amani bila Mungu, hiyo ni ya kitambo tu.

👉Ayubu 22:21 inasema "Mjue sana Mungu, ili uwe na AMANI; ndivyo MEMA yatavyokujia". Hakuna njia ya mkato ya kupata Amani ya kweli nje ya kutoa maisha yetu kwa Kristo, aliyekuja kumuokoa mwanadamu, na kumuweka huru na mishale ya Adui shetani, ambayo ni dhambi na matunda yake.

MUNGU ATAWALE NIA YA KILA MMOJA WATU ILI TUPATE USHINDI MILELE.

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA BARAKA TELE.

Na Ev. Eliezer Mwangosi.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, November 18, 2015

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeondoshwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kupangwa kwenye hatua ya makundi kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi baada ya kufungwa kwa magoli 7-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Mustapher Tchaker mjini Blida, Algeria

Stars imeondoshwa kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya kucheza michezo miwili, mchezo wa kwanza Stars ililazimishwa sare ya kufungana kwa goli 2-2 na Algeria jijini Dar es Salaam huku mchezo wa pili uliopigwa Blida, Algeria ukimalizika kwa Stars kulala kwa goli 7-0.

Algeria walianza kupata bao la kwanza sekunde ya 40 kupitia kwa Yacine Brahimi huku Ghoulam Faouzi akipachika goli la pili dakika ya 23 kabla ya Ryad Mahrez kutupia la tatu dakika ya 43 na kuufanya mchezo kwenda mapumziko Algeria wakiwa mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Farid Musa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela wakati Aishi Manula aliingia kuchukua nafasi ya Ali Mustafa.

Dakika ya 49 Algeria waliendeleza mvua ya magoli kwa Stars baada ya Slimani Islam kuipatia Algeria bao la nne kwa mkwaju wa penati wakati Ghoulam Faouzi akiifungia Algeria tano pia kwa mkwaju wa penati ikiwa ni dakika ya 59.
Carl Medjani akafunga goli la sita dakika ya 72 huku Slimani Islam akipachika bao la saba dakika ya 75.

Farid Musa, Himid Mao Mkami, Kelvin Yondani, Haji Mwinyi Nadir Haroub na Aishi Manula walioneshwa kadi ya njano huku Mudathir Yahya akioneshwa kadi mbili za njano zilizopelekea kupata kadi nyekundu dakika ya 41 kipindi cha kwanza na kuiacha Stars ikicheza pungufu kwa muda wote uliosalia.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.

Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November 17, 2015

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.

Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita, Bodi ilitoa orodha ya Awamu ya Tatu iliyokuwa na waombaji 6,915 waliopangiwa mikopo. Kati ya waombaji hao waliopangiwa mikopo, waombaji 4,642 ni walikua ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji 2,273 ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 48,469 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282; Awamu ya Pili wanafunzi 28,554; Awamu ya Tatu wanafunzi 6,915 na Awamu hii ya Nne wanafunzi 718 wamepangiwa mikopo.

Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

Mwisho. 


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
HONGERA MHESHIMIWA JOB NDUGAI KWA NAFASI HIYO
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, November 17, 2015

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
     Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa  “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako, nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania”  amesema malkia katika salamu zake.
     Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.  Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati,  mafanikio na furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.
     Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu  ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye amemtakia kheri  Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina  imani kuwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya uongozi wako kuelekea katika kupata maendeleo  na mafanikio zaidi”.  Amesema; na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo kuliletea sifa bara la Afrika.
     Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.
     “Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza kuwa  “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM  Mamlaka ya kuipeleka mbele Tanzania  kuelekea kwenye mafanikio zaidi”.  Ameongeza.
      Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya demokrasia barani Afrika.
     Naye Rais wa Jamhuri  ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio  katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.

……………………………………………MWISHO…………………………………………

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Novemba, 2015


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Mathayo 5:44-45 "Lakini mimi nawaambia, wapendeni ADUI zenu, waombeeni WANAOWAUDHI; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni....."

Nilipokuwa nafuatilia post za wapendwa wengi na wakati mwingine kusikiliza wakiongea juu ya matokeo ya uchaguzi hasa wa Uraisi, nimesikitika kugundua kwamba wapendwa wengi wameghafilika na kutanga mbali na misingi ya wokovu wetu. Wengi wameruhusu shina la uchungu lichipuke ndani ya mioyo yao na hatimaye kuwatia unajisi (Soma Waebrania 12:14-15), roho za visasi na uadui zimetawala kuwasumbua wengi.

Katika somo langu la 30.08.2015, nilitoa somo lililosema: WATU WA MUNGU NA SIASA / UCHAGUZI, likitoa mwanga jinsi Mungu anavyohusika na tawala za jamii, na watu wa Mungu wanachopaswa kukifanya na namna ya kuyapokea matokeo. Baada ya matokeo nimegundua watu wa Mungu wengi hawajui jinsi Mungu anavyotenda kazi hasa katika michakato ya kupata watawala wa serikali inayojumuisha WAOVU NA WEMA, mawazo ya Mungu yako tofauti sana na mawazo yetu. Hivyo tunapoona mambo hayako sawa, tunapaswa kutulia na kutafuta hekima yake.

Neno linasema "Mpende Adui na Kumuombea",  Jihoji Kama Mcha Mungu, baada ya matokeo ya uchaguzi na Raisi kuapishwa, iwe ni kwa haki au laa, umechukuwa hatua gani? Siku moja kabla ya Raisi kuapishwa nilisikia malalamiko mengi tena yenye uchungu na wengine kufikia kuombea Mabalaa yatokee ili asiapishwe. Hadi leo hii kuna wapendwa wengi wanaombea mabaya yatokee kwa Raisi aliye madarakani, ikiwa ni adhabu kutoka kwa Mungu. Kumbukeni Chama au Serikali haina Dini, ila ndani yake kuna wacha Mungu na Waovu. Kumbukeni Taifa la Israeli lilipigwa na kuhujumiwa haki na mataifa maovu kwa sababu tu ya maovu ya watu wachache.

KWA WATANZANIA: Wale wanaoamini kuwa wameporwa haki yao Kupitia mchakato wa uchaguzi, ni wakati wa kukaa na Mungu ili awape hekima ya kufanya maamuzi sahihi bila kutenda UOVU, wajichunguze na kujihoji, wakiona kuna uovu ndani yao juu ya jamii watubu na kuungama, ili Mungu ajidhihirishe juu yao kwa wakati. Waombeeni walioko madarakani kwa wakati huu, ili Mungu awape hekima na ufahamu wa kutenda mambo kwa HAKI. Kusudi la Mungu ni KUOKOA sio kupoteza roho, ombea waokolewe, wawe na hofu ya Mungu, ndipo mtapandishwa juu ya Vilima kwa wakati uliokubalika.

KWA WATANZANIA: Wanaoamini wameshinda kwenye uchaguzi; kwa hakika Mungu ndiye anayejua, kama ni kwa uhalali au laa. Kama nilivyotangulia kusema, ndani ya vyama na serikali kuna WAOVU na WEMA. Ikitokea Mungu ameruhusu mafanikio kwa njia isiyo halali, sio kwamba anakubaliana na uovu, ila kuna neema inamtafuta mmoja atubu, ili aokolewe. Huu ni wakati wa mpito wa kupimwa tena katika mizania ya Mungu. Kama kuna Uovu wowote ni wakati wa Kutubu ili Mungu awafanikishe katika HAKI. Kumbukeni hakuna AMANI Kwa Waovu (Isaya 48:22).

Kama ushindi ulikuwa ni wa halali, bado mnatakiwa kunyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili azidi kuwakweza na kuwafikisha katika vilele. Bila Mungu hekima ya Mwanadamu ni patupu, shetani atawashinda na kuwa na hali mbaya kuliko matazamio ya watanzania. 1Petro 5:6-7.

HITIMISHO: Bwana Mungu anasema "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA" Isaya 55:8. Watu wa Mungu tunahitaji kuwa makini na kuomba hekima kwa Mungu, hasa tunapojihusisha na mambo ya Vyama vya siasa ambavyo havina misingi ya Dini. Sisi tunatazama kwa macho ili kutimiza makusudi na mapenzi ya mioyo yetu, lakini Mungu hayuko hivyo. Usishindwe na Ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema 'Warumi 12:21'.

Watu wa Mungu tunaoishi katika kazazi hiki kiovu, tunapaswa kuwa chachu ya kuleta AMANI, tukiwaombea waovu waokolewe, kuchukia UOVU sio kulipa visasi na kuombea mabaya, hizo ni roho za yule adui. Waovu wanaonywa kwa upendo, wanashauriwa, wanaombewa, wakiendelea na uovu unaotudhuru tutatumia vyombo vya sheria na kutafuta haki. Ni agizo la Mungu kuzitii Mamlaka zozote zilizowekwa katika Jamii - Warumi 13:1-7. Mwenye Mamlaka ya mwisho juu ya Kuziweka na Kuziangusha Mamlaka ni Mungu, kwa njia zozote mwanadamu hawezi bila Mungu.

MUNGU BARIKI TANZANIA - TIMIZA KUSUDI LAKO KWA WATANZANIA - KATUONDOLEE UOVU - KILA ALIYESHIKA MAMLAKA UKAMTIISHE AKAWE CHINI YA MAMLAKA YAKO - VIONGOZI WOTE UWABARIKI NA KUWAPA HEKIMA YA KUONGOZA TAIFA LA TANZANIA KWA WAKATI ULIO AMRIWA.

Na Ev. Eliezer Mwangosi - Tel. 0767210299 - Email. eliezer.mwangosi@yahoo.com.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Saturday, November 14, 2015

Juma hili lilianza siku ya jumapili tarehe 8/11/2015 na kuhimishwa leo kukiwa na mada mbalimbali za kujenga kanisa hasa ndani ya familia zetu. Juma hili liliendeshwa na Mama Neema Tuvako kutoka Morogoro na leo juma hili linahitimishwa huku wito ukiwa ni kufanya kazi ya Mungu kwa umoja ndani ya Kanisa bila kuangalia jinsia kwani wote hutegemeana.




Picha na Eliya Kisika
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA